1 Samuel 11:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, Shauli alikuwa anatoka shambani akiwa na fahali wake, akauliza, “Watu wana nini? Kwa nini wanalia?” Wakamwambia habari waliyoleta wajumbe kutoka Yabeshi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo huo Sauli alikuwa anarudi kutoka mashambani, akiwa nyuma ya maksai wake, naye akauliza, “Watu wana nini? Mbona wanalia?” Ndipo wakamweleza vile wanaume wa Yabeshi walivyokuwa wamesema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, Sauli akaja akifuata ng'ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, Shauli alikuwa anatoka shambani akiwa na fahali wake, akauliza, “Watu wana nini? Kwa nini wanalia?” Wakamwambia habari waliyoleta wajumbe kutoka Yabeshi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo huo Sauli alikuwa anarudi kutoka mashambani, akiwa nyuma ya maksai wake, naye akauliza, “Watu wana nini? Mbona wanalia?” Ndipo wakamweleza jinsi watu wa Yabeshi walivyokuwa wamesema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo huo Sauli alikuwa anarudi kutoka mashambani, akiwa nyuma ya maksai wake, naye akauliza, “Watu wana nini? Mbona wanalia?” Ndipo wakamweleza jinsi watu wa Yabeshi walivyokuwa wamesema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, Sauli akaja akifuata ng'ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, Shauli alikuwa anatoka shambani akiwa na fahali wake, akauliza, “Watu wana nini? Kwa nini wanalia?” Wakamwambia habari waliyoleta wajumbe kutoka Yabeshi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Sauli alikuwa anarudi malishoni akiwafuata ng'ombe; hapo Sauli akauliza: Watu wanalilia nini? Wakamsimulia habari, watu wa Yabesi walizozileta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, Sauli akaja akifuata ng’ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, Saulo alikuwa anatoka kwenye shamba akiwa na ngombe dume wake, akauliza: “Watu wana nini? Kwa nini wanalia?” Wakamwambia habari wajumbe waliyoleta kutoka Yabesi.