1 Samuel 11:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akachukua fahali wawili akawakatakata vipandevipande, akatuma wajumbe wavipitishe kila mahali nchini Israeli wakisema, “Mtu yeyote ambaye hatamfuata Shauli na Samueli vitani, fahali wake watafanywa hivyo.” Hofu ikawaaingia Waisraeli kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu angeweza kufanya. Kwa hiyo, wote walitoka kwa pamoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akachukua maksai wawili na kuwakata vipande vipande, naye kuvituma hivyo vipande kupitia wajumbe katika Israeli yote, wakitangaza, “Hivi ndivyo itakavyofanyika kwa maksai wa kila mmoja ambaye hatamfuata Sauli na Samweli.” Kisha kicho cha Mwenyezi Mungu kikawaangukia watu, nao wakatoka kama mtu mmoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akatwaa jozi ya ng'ombe, akawakata-kata vipande, kisha akavipeleka vile vipande mipakani mwote mwa Israeli kwa mikono ya wajumbe, kusema, Ye yote asiyetoka nyuma ya Sauli na Samweli, ng'ombe zake watatendwa vivi hivi. Basi utisho wa Bwana ukawaangukia wale watu, wakatoka kama mtu mmoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akachukua fahali wawili akawakatakata vipandevipande, akatuma wajumbe wavipitishe kila mahali nchini Israeli wakisema, “Mtu yeyote ambaye hatamfuata Shauli na Samueli vitani, fahali wake watafanywa hivyo.” Hofu ikawaaingia Waisraeli kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu angeweza kufanya. Kwa hiyo, wote walitoka kwa pamoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akachukua jozi ya maksai na kuwakata vipande vipande, naye kuvituma hivyo vipande kupitia wajumbe katika Israeli yote, wakitangaza, “Hivi ndivyo itakavyofanyika kwa maksai wa kila mmoja ambaye hatamfuata Sauli na Samweli.” Kisha hofu ya BWANA ikawaangukia watu, nao wakatoka kama mtu mmoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akachukua jozi ya maksai na kuwakata vipande vipande, naye kuvituma hivyo vipande kupitia wajumbe katika Israeli yote, wakitangaza, “Hivi ndivyo itakavyofanyika kwa maksai wa kila mmoja ambaye hatamfuata Sauli na Samweli.” Kisha hofu ya bwana ikawaangukia watu, nao wakatoka kama mtu mmoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akachukua fahali wawili waliofungwa nira, akawakatakata vipande, kisha akawatuma wajumbe kuvipeleka vile vipande kote katika Israeli, wakisema, Yeyote ambaye hatamfuata Sauli na Samweli, ng'ombe wake watafanyiwa vivi hivi. Basi utisho wa BWANA ukawaangukia wale watu, wakatoka kwa pamoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akachukua fahali wawili akawakatakata vipandevipande, akatuma wajumbe wavipitishe kila mahali nchini Israeli wakisema, “Mtu yeyote ambaye hatamfuata Shauli na Samueli vitani, fahali wake watafanywa hivyo.” Hofu ikawaaingia Waisraeli kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu angeweza kufanya. Kwa hiyo, wote walitoka kwa pamoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akakamata ng'ombe wawili, akawakatakata, akawatuma wale wajumbe kwenda katika nchi zote za Waisiraeli na kuwapelekea watu vipande vya nyama kwamba: Kila mtu asiyetoka kumfuata Sauli na Samweli ng'ombe wake watafanyiziwa hivyo. Ndipo, watu walipoguiwa na kituko cha Bwana, wakatoka kama mtu mmoja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akatwaa jozi ya ng’ombe, akawakata-kata vipande, kisha akavipeleka vile vipande mipakani mwote mwa Israeli kwa mikono ya wajumbe, kusema, Ye yote asiyetoka nyuma ya Sauli na Samweli, ng’ombe zake watatendwa vivi hivi. Basi utisho wa BWANA ukawaangukia wale watu, wakatoka kama mtu mmoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akatwaa ngombe dume wawili, akawakatakata vipande, akatuma wajumbe wapitishe vipande hivyo katika mipaka yote ya Waisraeli wakisema: “Mutu yeyote ambaye hatamufuata Saulo na Samweli katika vita, ngombe dume wake watafanyiwa hivyo.” Waisraeli waliingiwa na hofu juu ya kile ambacho Yawe angeweza kufanya. Kwa hiyo, wote walitoka pamoja.