1 Samuel 12:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo wakamwambia Samueli, “Tafadhali utuombee sisi watumishi wako kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili tusife; kwa sababu tumezidisha dhambi zetu kwa uovu huo wa kujitakia mfalme.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wote wakamwambia Samweli, “Mwombe Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa ajili ya watumishi wako, ili tusije tukafa, kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wote wakamwambia Samweli, Utuombee sisi watumwa wako kwa Bwana, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo wakamwambia Samueli, “Tafadhali utuombee sisi watumishi wako kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili tusife; kwa sababu tumezidisha dhambi zetu kwa uovu huo wa kujitakia mfalme.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wote wakamwambia Samweli, “Mwombe BWANA Mungu wako kwa ajili ya watumishi wako, ili tusije tukafa, kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wote wakamwambia Samweli, “Mwombe bwana Mwenyezi Mungu wako kwa ajili ya watumishi wako, ili tusije tukafa, kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wote wakamwambia Samweli, Tuombee watumishi wako kwa BWANA, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo wakamwambia Samueli, “Tafadhali utuombee sisi watumishi wako kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili tusife; kwa sababu tumezidisha dhambi zetu kwa uovu huo wa kujitakia mfalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha watu wote wakamwambia Samweli: Waombee watumishi wako kwake Bwana Mungu wako, tusife! Kwani makosa yetu yote tumeyaongeza na kibaya hiki cha kujitakia mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wote wakamwambia Samweli, Utuombee sisi watumwa wako kwa BWANA, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo wakamwambia Samweli: “Tafazali, utuombee sisi watumishi wako kwa Yawe, Mungu wako, kusudi tusikufe; kwa sababu tumezidisha zambi zetu kwa uovu huo wa kujitakia mufalme.”