1 Samuel 12:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena kwa upande wangu haitatokea niache kuwaombea kwa Mwenyezi-Mungu; kufanya hivyo itakuwa kumkosea Mwenyezi-Mungu. Nitaendelea kuwafundisha njia njema na ya haki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini iwe mbali nami kutenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu kwa kushindwa kuwaombea. Mimi nitawafundisha njia iliyo njema na nyoofu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena kwa upande wangu haitatokea niache kuwaombea kwa Mwenyezi-Mungu; kufanya hivyo itakuwa kumkosea Mwenyezi-Mungu. Nitaendelea kuwafundisha njia njema na ya haki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa habari yangu, iwe mbali nami kutenda dhambi dhidi ya BWANA kwa kushindwa kuwaombea. Mimi nitawafundisha njia iliyo njema na ya kunyooka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa habari yangu, iwe mbali nami kutenda dhambi dhidi ya bwana kwa kushindwa kuwaombea. Mimi nitawafundisha njia iliyo njema na ya kunyooka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena kwa upande wangu haitatokea niache kuwaombea kwa Mwenyezi-Mungu; kufanya hivyo itakuwa kumkosea Mwenyezi-Mungu. Nitaendelea kuwafundisha njia njema na ya haki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nami hili na liniendee mbali, nisimkosee Bwana nikiacha kuwaombea! Ila nitawafundisha kuishika njia njema inyokayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena kwa upande wangu haitatokea niache kuwaombea kwa Yawe; kufanya hivyo itakuwa kumukosea Yawe. Nitaendelea kuwafundisha njia njema na ya haki.