1 Samuel 12:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niko hapa, na kama nimefanya tendo lolote lile baya, basi, toeni ushahidi mbele ya Mwenyezi-Mungu na mbele ya mfalme wake mteule. Je, nimepora fahali au punda wa mtu yeyote? Je, nimempunja mtu yeyote? Je, nimemkandamiza mtu yeyote? Je, nimepokea rushwa kwa mtu yeyote ili kupotosha haki? Nami nitamrudishia chochote kile.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi ninasimama hapa. Shuhudieni dhidi yangu mbele za Mwenyezi Mungu na mpakwa mafuta wake. Nimechukua maksai wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimepata kumdanganya? Nimemdhulumu nani? Nimepokea rushwa kutoka kwa nani ili nifumbe macho yangu? Kama nimefanya chochote katika hivi, nitawarudishia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za Bwana, na mbele ya masihi
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niko hapa, na kama nimefanya tendo lolote lile baya, basi, toeni ushahidi mbele ya Mwenyezi-Mungu na mbele ya mfalme wake mteule. Je, nimepora fahali au punda wa mtu yeyote? Je, nimempunja mtu yeyote? Je, nimemkandamiza mtu yeyote? Je, nimepokea rushwa kwa mtu yeyote ili kupotosha haki? Nami nitamrudishia chochote kile.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi ninasimama hapa. Shuhudieni juu yangu mbele za BWANA na mpakwa mafuta wake. Nimechukua maksai wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimepata kumdanganya? Ni nani nimepata kumwonea? Ni kutoka kwenye mkono wa nani nimepokea rushwa ili kunifanya nifumbe macho yangu? Kama nimefanya cho chote katika hivi, mimi nitawarudishia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi ninasimama hapa. Shuhudieni juu yangu mbele za bwana na mpakwa mafuta wake. Nimechukua maksai wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimepata kumdanganya? Ni nani nimepata kumwonea? Ni kutoka kwenye mkono wa nani nimepokea rushwa ili kunifanya nifumbe macho yangu? Kama nimefanya chochote katika hivi, mimi nitawarudishia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za BWANA, na mbele ya masihi wake, nilitwaa ng'ombe wa nani? Au nilitwaa punda wa nani? Au ni nani niliyemdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niko hapa, na kama nimefanya tendo lolote lile baya, basi, toeni ushahidi mbele ya Mwenyezi-Mungu na mbele ya mfalme wake mteule. Je, nimepora fahali au punda wa mtu yeyote? Je, nimempunja mtu yeyote? Je, nimemkandamiza mtu yeyote? Je, nimepokea rushwa kwa mtu yeyote ili kupotosha haki? Nami nitamrudishia chochote kile.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, nitazameni, mniumbue mbele ya Bwana na mbele ya mtu wake, aliyempaka mafuta, kama nimechukua ng'ombe wa mtu, au kama nimechukua punda wa mtu, au kama nimekorofisha mtu, au kama nimeponda mtu, au kama nimechukua mkononi mwa mtu fedha za kupenyezewa za kuyapofusha macho yangu! Kama ndivyo, nitawarudishia ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za BWANA, na mbele ya masihi wake, nalitwaa ng’ombe wa nani? Au nalitwaa punda wa nani? Au ni nani niliyemdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niko hapa, na kama nimefanya tendo lolote baya, basi, mutoe ushuhuda mbele ya Yawe na mbele ya mufalme wake muchaguliwa. Nimenyanganya ngombe dume au punda wa mutu yeyote? Nimemugandamiza mutu yeyote? Nimemutesa mutu yeyote? Nimepokea kituliro kwa mutu yeyote kusudi nifunge macho mbele ya matendo yake? Museme nami nitamurudishia kitu chochote kile.”