1 Samuel 12:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Samueli akajibu, “Mwenyezi-Mungu ni shahidi juu yenu, na mfalme wake mteule leo ni shahidi kuwa mmeniona sina hatia.” Wao wakajibu: “Yeye ni shahidi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Samweli akawaambia, “Mwenyezi Mungu ni shahidi dhidi yenu, pia mpakwa mafuta wake ni shahidi siku hii ya leo, kwamba hamkukuta chochote mkononi mwangu.” Wakasema, “Yeye ni shahidi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Bwana ni shahidi juu yenu, na masihi
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Samueli akajibu, “Mwenyezi-Mungu ni shahidi juu yenu, na mfalme wake mteule leo ni shahidi kuwa mmeniona sina hatia.” Wao wakajibu: “Yeye ni shahidi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Samweli akawaambia, “BWANA ni shahidi juu yenu, pia mpakwa mafuta wake ni shahidi siku hii ya leo, kwamba hamkukuta cho chote mkononi mwangu.” Wakasema, “Yeye ni shahidi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Samweli akawaambia, “ bwana ni shahidi juu yenu, pia mpakwa mafuta wake ni shahidi siku hii ya leo, kwamba hamkukuta chochote mkononi mwangu.” Wakasema, “Yeye ni shahidi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, BWANA ni shahidi juu yenu, na masihi wake ni shahidi leo, ya kuwa hamkuona kitu mkononi mwangu. Nao wakasema, Yeye ni shahidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Samueli akajibu, “Mwenyezi-Mungu ni shahidi juu yenu, na mfalme wake mteule leo ni shahidi kuwa mmeniona sina hatia.” Wao wakajibu: “Yeye ni shahidi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipowaambia: Siku hii ya leo Bwana ni shahidi wangu kwenu, naye aliyempaka mafuta ni shahidi wangu, ya kuwa hamkuona cho chote mkononi mwangu. Wakasema: Kweli, ndiye shahidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, BWANA ni shahidi juu yenu, na masihi wake ni shahidi leo, ya kuwa hamkuona kitu mkononi mwangu. Nao wakasema, Yeye ni shahidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Samweli akajibu: “Yawe ni mushuhuda juu yenu, na mufalme wake muchaguliwa leo ni mushuhuda kuwa mumeniona sina kosa.” Wao wakajibu: “Yeye ni mushuhuda.”