1 Samuel 12:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Yakobo na jamaa yake walipokwenda Misri, na Wamisri walipowakandamiza, babu zenu walimlilia Mwenyezi-Mungu; naye akawatuma Mose na Aroni ambao waliwatoa babu zenu nchini Misri na kuwafanya mkae katika nchi hii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Baada ya Yakobo kuingia Misri, walimlilia Mwenyezi Mungu awasaidie, naye Mwenyezi Mungu akawatuma Musa na Haruni, ambao waliwatoa baba zenu kutoka Misri na kuwakalisha mahali hapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia Bwana, ndipo Bwana akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Yakobo na jamaa yake walipokwenda Misri, na Wamisri walipowakandamiza, babu zenu walimlilia Mwenyezi-Mungu; naye akawatuma Mose na Aroni ambao waliwatoa babu zenu nchini Misri na kuwafanya mkae katika nchi hii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Baada ya Yakobo kuingia Misri, walimlilia BWANA kwa ajili ya msaada, naye BWANA akawatuma Mose na Aroni, ambao waliwatoa baba zenu kutoka Misri na kuwakalisha mahali hapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Baada ya Yakobo kuingia Misri, walimlilia bwana kwa ajili ya msaada, naye bwana akawatuma Musa na Haruni, ambao waliwatoa baba zenu kutoka Misri na kuwakalisha mahali hapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia BWANA, ndipo BWANA akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Yakobo na jamaa yake walipokwenda Misri, na Wamisri walipowakandamiza, babu zenu walimlilia Mwenyezi-Mungu; naye akawatuma Mose na Aroni ambao waliwatoa babu zenu nchini Misri na kuwafanya mkae katika nchi hii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yakobo alipoingia Misri, baba zenu walipomlilia Bwana, Bwana akamtuma Mose na Haroni, akawatoa baba zenu huko Misri, akawakalisha mahali hapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia BWANA, ndipo BWANA akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Yakobo na jamaa yake walipokwenda Misri, na Wamisri walipowagandamiza, babu zenu walimulilia Yawe. Naye akawatuma Musa na Haruni ambao waliwatoa babu zenu katika inchi ya Misri na kuwafanya mukae katika inchi hii.