1 Samuel 13:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sasa ufalme wako hautadumu kwa kuwa amri aliyokuamuru Mwenyezi-Mungu hukuitii. Mwenyezi-Mungu amejitafutia mtu mwingine ambaye atamtii kwa moyo wote, na huyo ndiye ambaye amemteua kuwa mtawala juu ya watu wake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa ufalme wako hautadumu; Mwenyezi Mungu amemtafuta mtu aupendezaye moyo wake, na amemchagua awe kiongozi wa watu wake, kwa sababu hukuyatii maagizo ya Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sasa ufalme wako hautadumu; Bwana amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye Bwana amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile Bwana alilokuamuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sasa ufalme wako hautadumu kwa kuwa amri aliyokuamuru Mwenyezi-Mungu hukuitii. Mwenyezi-Mungu amejitafutia mtu mwingine ambaye atamtii kwa moyo wote, na huyo ndiye ambaye amemteua kuwa mtawala juu ya watu wake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amemtafuta mtu aupendezae moyo wake, na amemchagua awe kiongozi wa watu wake, kwa sababu hukuyatii maagizo ya BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa ufalme wako hautadumu; bwana amemtafuta mtu aupendezaye moyo wake, na amemchagua awe kiongozi wa watu wake, kwa sababu hukuyatii maagizo ya bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye BWANA amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile BWANA alilokuamuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sasa ufalme wako hautadumu kwa kuwa amri aliyokuamuru Mwenyezi-Mungu hukuitii. Mwenyezi-Mungu amejitafutia mtu mwingine ambaye atamtii kwa moyo wote, na huyo ndiye ambaye amemteua kuwa mtawala juu ya watu wake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sasa ufalme wako hausimamiki, Bwana amekwisha kujitafutia mtu mwingine aupendezaye moyo wake, naye amemwagiza kuwa mkuu wao walio ukoo wake, kwani hukuyaangalia, Bwana aliyokuagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye BWANA amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile BWANA alilokuamuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa ufalme wako hautadumu kwa sababu amri Yawe aliyokuamuru haukuitii. Yawe amejitafutia mutu mwingine ambaye atamutii kwa moyo wote, na huyo ndiye ambaye atamuchagua kuwa mutawala juu ya watu wake.”