1 Samuel 13:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo hapakuwepo na mhunzi yeyote katika nchi nzima ya Israeli, kwani Wafilisti walikusudia kuwazuia Waebrania wasije wakajitengenezea mapanga au mikuki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hapakuwa na mhunzi ambaye angeweza kupatikana katika nchi yote ya Israeli, kwa sababu Wafilisti walikuwa wamesema, “Waebrania wasije wakatengeneza panga au mikuki!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, hakuonekana mhunzi ye yote katika nchi yote ya Israeli; kwa kuwa Wafilisti walisema, Waebrania wasije wakajifanyizia panga au mikuki;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo hapakuwepo na mhunzi yeyote katika nchi nzima ya Israeli, kwani Wafilisti walikusudia kuwazuia Waebrania wasije wakajitengenezea mapanga au mikuki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hapakuwa na mhunzi ambaye angeweza kupatikana katika nchi yote ya Israeli, kwa sababu Wafilisti walikuwa wamesema, “Waebrania wasije wakatengeneza panga au mikuki!.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hapakuwa na mhunzi ambaye angeweza kupatikana katika nchi yote ya Israeli, kwa sababu Wafilisti walikuwa wamesema, “Waebrania wasije wakatengeneza panga au mikuki!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, hakukuwa mhunzi yeyote katika nchi yote ya Israeli; kwa kuwa Wafilisti walisema, Waebrania wasije wakajitengenezea panga au mikuki;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo hapakuwepo na mhunzi yeyote katika nchi nzima ya Israeli, kwani Wafilisti walikusudia kuwazuia Waebrania wasije wakajitengenezea mapanga au mikuki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika nchi yote ya Waisiraeli hakuonekana mhunzi, kwani Wafilisti walisema: Waebureo wasijifanyie wala panga wala mikuki!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, hakuonekana mhunzi ye yote katika nchi yote ya Israeli; kwa kuwa Wafilisti walisema, Waebrania wasije wakajifanyizia panga au mikuki;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo hakukuwa mufuaji yeyote wa vyuma katika inchi nzima ya Israeli, maana Wafilistini walikusudia kuwazuia Waebrania wasipate kujitengenezea mapanga au mikuki.