1 Samuel 13:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli walikuwa wanalipa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa wembe wa plau na sururu. Na bei ya kunoa shoka au kupata mchokoo ilikuwa theluthi moja ya shekeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bei ilikuwa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa majembe ya plau na majembe ya mkono, na theluthi moja ya shekeli kunoa uma, na shoka, na mchokoo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ila walikuwa na tupa za kunolea sululu, na miundu, na mauma, na mashoka; na kwa kuinoa michokoo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli walikuwa wanalipa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa wembe wa plau na sururu. Na bei ya kunoa shoka au kupata mchokoo ilikuwa theluthi moja ya shekeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bei ilikuwa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa majembe ya plau na majembe ya mkono, na theluthi moja ya shekeli kwa nyuma, mashoka na michokoo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bei ilikuwa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa majembe ya plau na majembe ya mkono, na theluthi moja ya shekeli kwa nyuma, mashoka na michokoo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na walilipa theluthi mbili za shekeli kunoa jembe na miundu, na theluthi moja ya shekeli kunoa mashoka na kuchonga michokoo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli walikuwa wanalipa fedha theluthi mbili za shekeli kunoa wembe wa plau na sururu. Na bei ya kunoa shoka au kupata mchokoo ilikuwa theluthi moja ya shekeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
makali ya majembe au ya miundu au ya pembe za uma au ya mashoka yakidugika, hata wakitaka tu kunyosha ncha za fimbo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ila walikuwa na tupa za kunolea sululu, na miundu, na mauma, na mashoka; na kwa kuinoa michokoo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli walikuwa wanalipa feza sehemu mbili ya tatu za shekeli kwa kunoa majembe na sururu. Na bei ya kunoa shoka au kuchongoa chuma ilikuwa sehemu moja ya tatu ya shekeli.