1 Samuel 13:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafilisti walikuwa na magari 30,000, askari 6,000 wapandafarasi na kikosi cha askari wa miguu wengi kama mchanga wa pwani; wote walipanda juu na kupiga kambi yao huko Mikmashi, mashariki ya Beth-aveni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wafilisti wakakusanyika ili kupigana na Israeli, wakiwa na magari ya vita elfu tatu, waendesha magari ya vita elfu sita, na askari wa miguu wengi kama mchanga wa ufuoni mwa bahari. Walipanda na kupiga kambi huko Mikmashi, mashariki mwa Beth-Aveni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao Wafilisti wakakusanyana ili wapigane na Waisraeli, magari thelathini elfu, na wapanda farasi sita elfu, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafilisti walikuwa na magari 30,000, askari 6,000 wapandafarasi na kikosi cha askari wa miguu wengi kama mchanga wa pwani; wote walipanda juu na kupiga kambi yao huko Mikmashi, mashariki ya Beth-aveni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wafilisti wakakusanyika ili kupigana na Israeli, wakiwa na magari ya vita 3,000, waendesha magari ya vita 6,000 na askari wa miguu wengi kama mchanga wa ufuoni mwa bahari. Walipanda na kupiga kambi huko Mikmashi, mashariki ya Beth-Aveni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wafilisti wakakusanyika ili kupigana na Israeli, wakiwa na magari ya vita 3,000, waendesha magari ya vita 6,000 na askari wa miguu wengi kama mchanga wa ufuoni mwa bahari. Walipanda na kupiga kambi huko Mikmashi, mashariki ya Beth-Aveni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao Wafilisti wakakusanyika ili wapigane na Waisraeli, magari elfu thelathini, na wapanda farasi elfu sita, na watu kama mchanga ulio ufukweni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafilisti walikuwa na magari 30,000, askari 6,000 wapandafarasi na kikosi cha askari wa miguu wengi kama mchanga wa pwani; wote walipanda juu na kupiga kambi yao huko Mikmashi, mashariki ya Beth-aveni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wafilisti nao wakakusanyika kupigana na Waisiraeli; magari 30000 na wapanda farasi 6000, nao watu wao wakawa wengi kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari. Hao wakapanda, wakapiga makambi kule Mikimasi kuelekea Beti-Aweni, ni upande wake wa maawioni kwa jua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao Wafilisti wakakusanyana ili wapigane na Waisraeli, magari thelathini elfu, na wapanda farasi sita elfu, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafilistini walikuwa na magari elfu makumi tatu, waaskari elfu sita wapanda-farasi na kikundi cha waaskari wa miguu wengi kama muchanga wa bahari. Wote walipanda juu na kupiga kambi yao kule Mikimasi, upande wa mashariki wa Beti-Aweni.