1 Samuel 14:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafilisti waliokuwa kwenye ngome wakamwita Yonathani na kijana aliyembebea silaha, “Njoni huku kwetu, nasi tutawaonesha kitu.” Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha, “Nifuate; Mwenyezi-Mungu amewatia mikononi mwa Israeli.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanaume wa kwenye doria wakawapazia sauti Yonathani na mbeba silaha wake, wakisema, “Njooni, pandeni kwetu, nasi tutawakomesha.” Basi Yonathani akamwambia mbeba silaha wake, “Panda nyuma yangu; Mwenyezi Mungu amewatia mikononi mwa Israeli.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watu wa ngomeni wakamjibu Yonathani na mchukua silaha zake, wakasema, Haya! Ninyi, pandeni juu hapa tulipo, na sisi tutawaonyesha jambo. Yonathani akamwambia yule aliyezichukua silaha, Haya! Panda nyuma yangu; kwa kuwa Bwana amewatia mikononi mwa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafilisti waliokuwa kwenye ngome wakamwita Yonathani na kijana aliyembebea silaha, “Njoni huku kwetu, nasi tutawaonesha kitu.” Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha, “Nifuate; Mwenyezi-Mungu amewatia mikononi mwa Israeli.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa kwenye doria wakawapigia kelele Yonathani na mbeba silaha wake, wakisema, “Njoni pandeni kwetu nasi tutawakomesha.” Basi Yonathani akamwambia mbeba silaha wake, “Panda nyuma yangu, BWANA amewatia mikononi mwa Israeli.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa kwenye doria wakawapigia kelele Yonathani na mbeba silaha wake, wakisema, “Njooni, pandeni kwetu nasi tutawakomesha.” Basi Yonathani akamwambia mbeba silaha wake, “Panda nyuma yangu; bwana amewatia mikononi mwa Israeli.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watu wa ngomeni wakamjibu Yonathani na mbebaji wa silaha zake, wakasema, Haya! Ninyi, pandeni juu hapa tulipo, na sisi tutawaonesha jambo. Yonathani akamwambia yule aliyezichukua silaha, Haya! Panda nyuma yangu; kwa kuwa BWANA amewatia mikononi mwa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafilisti waliokuwa kwenye ngome wakamwita Yonathani na kijana aliyembebea silaha, “Njoni huku kwetu, nasi tutawaonesha kitu.” Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha, “Nifuate; Mwenyezi-Mungu amewatia mikononi mwa Israeli.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wale watu wa zamu wakaanza kusema naye Yonatani na mchukua mata yake wakiwaambia: Tupandieni, tuwajulishe neno! Ndipo, Yonatani alipomwambia mchukua mata yake: Panda nyuma yangu! Kwani Bwana amewatia mikononi mwa Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watu wa ngomeni wakamjibu Yonathani na mchukua silaha zake, wakasema, Haya! Ninyi, pandeni juu hapa tulipo, na sisi tutawaonyesha jambo. Yonathani akamwambia yule aliyezichukua silaha, Haya! Panda nyuma yangu; kwa kuwa BWANA amewatia mikononi mwa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafilistini waliokuwa kwenye kambi wakamwita Yonatani na kijana aliyemubebea silaha: “Mukuje huku kwetu, nasi tutawaonyesha kitu.” Yonatani akamwambia yule kijana aliyemubebea silaha: “Unifuate. Yawe amewatia katika mikono ya Waisraeli.”