1 Samuel 14:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ahiya, mwana wa Ahitubu ndugu yake Ikabodi mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa Mwenyezi-Mungu mjini Shilo, alikuwa ndiye aliyevaa kizibao cha kuhani. Watu hawakujua kwamba Yonathani amekwisha ondoka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
miongoni mwao alikuwepo Ahiya, aliyekuwa amevaa kizibau. Alikuwa mwana wa Ikabodi, nduguye Ahitubu mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa Mwenyezi Mungu huko Shilo. Hakuna yeyote aliyekuwa na habari kwamba Yonathani alikuwa ameondoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na Ahiya, mwana wa Ahitubu nduguye Ikabodi, mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa Bwana huko Shilo, mwenye kuvaa naivera. Tena hao watu hawakujua ya kwamba Yonathani ameondoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ahiya, mwana wa Ahitubu ndugu yake Ikabodi mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa Mwenyezi-Mungu mjini Shilo, alikuwa ndiye aliyevaa kizibao cha kuhani. Watu hawakujua kwamba Yonathani amekwisha ondoka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
miongoni mwao alikuwepo Ahiya, ambaye alikuwa amevaa kisibau. Alikuwa mwana wa Ikabodi, nduguye Ahitubu mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa BWANA huko Shilo. Hakuna ye yote aliyekuwa na habari kwamba Yonathani alikuwa ameondoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
miongoni mwao alikuwepo Ahiya, ambaye alikuwa amevaa kisibau. Alikuwa mwana wa Ikabodi, nduguye Ahitubu mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa bwana huko Shilo. Hakuna yeyote aliyekuwa na habari kwamba Yonathani alikuwa ameondoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
pamoja na Ahiya, mwana wa Ahitubu nduguye Ikabodi, mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa BWANA huko Shilo, aliyevaa naivera. Tena hao watu hawakujua ya kwamba Yonathani ameondoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ahiya, mwana wa Ahitubu ndugu yake Ikabodi mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa Mwenyezi-Mungu mjini Shilo, alikuwa ndiye aliyevaa kizibao cha kuhani. Watu hawakujua kwamba Yonathani amekwisha ondoka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Ahia, mwana wa Ahitubu, ndugu ya Ikabodi, mwana wa Pinehasi, mwana wa Eli aliyekuwa mtambikaji wa Bwana huko Silo, ndiye aliyevaa kisibau cha mtambikaji. Hata watu hawakujua, ya kuwa Yonatani amekwenda zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na Ahiya, mwana wa Ahitubu nduguye Ikabodi, mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa BWANA huko Shilo, mwenye kuvaa naivera. Tena hao watu hawakujua ya kwamba Yonathani ameondoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ahiya mwana wa Ahitubu ndugu yake na Ikabodi mwana wa Finehasi mujukuu wa Eli kuhani wa Yawe katika muji wa Shilo, alikuwa ndiye aliyevaa kizibao cha kuhani. Watu hawakujua kwamba Yonatani amekwisha ondoka.