1 Samuel 14:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawaambia, “Nendeni mkawaambie watu wote walete ng'ombe na kondoo wao hapa, wawachinje na kuwala hapa. Wasitende dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, kwa kula nyama yenye damu.” Hivyo, usiku ule wote walipeleka ng'ombe wao na kuwachinjia hapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Sauli akasema, “Nendeni miongoni mwa watu, mwaambie, ‘Kila mmoja wenu aniletee ng’ombe wake na kondoo, mwachinjie hapa na mle. Msitende dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu kwa kula nyama ikiwa na damu ndani yake.’ ” Hivyo kila mmoja akaleta ng’ombe wake jioni ile na kumchinja hapo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Sauli akasema, Haya! Tawanyikeni katikati ya watu mkawaambie, Nileteeni hapa kila mtu ng'ombe wake, na kila mtu kondoo wake, mkawachinje hapa na kula; wala msikose juu ya Bwana, kwa kula pamoja na damu. Nao watu wote wakaleta kila mtu ng'ombe wake pamoja naye usiku ule, nao wakawachinja hapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawaambia, “Nendeni mkawaambie watu wote walete ng'ombe na kondoo wao hapa, wawachinje na kuwala hapa. Wasitende dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, kwa kula nyama yenye damu.” Hivyo, usiku ule wote walipeleka ng'ombe wao na kuwachinjia hapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akasema, “Nendeni miongoni mwa watu na waambieni, ‘Kila mmoja wenu aniletee ng'ombe wake na kondoo, wachinjeni hapa na mle. Msitende dhambi dhidi ya BWANA, kwa kula nyama ikiwa na damu ndani yake.’ ” Hivyo kila mmoja akaleta ng'ombe wake jioni ile na kumchinja hapo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Sauli akasema, “Nendeni miongoni mwa watu, mwaambie, ‘Kila mmoja wenu aniletee ng’ombe wake na kondoo, mwachinjie hapa na mle. Msitende dhambi dhidi ya bwana kwa kula nyama ikiwa na damu ndani yake.’ ” Hivyo kila mmoja akaleta ng’ombe wake jioni ile na kumchinja hapo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Sauli akasema, Haya! Tawanyikeni katikati ya watu mkawaambie, Nileteeni hapa kila mtu ng'ombe wake, na kila mtu kondoo wake, mkawachinje hapa na kula; wala msikose juu ya BWANA, kwa kula pamoja na damu. Nao watu wote wakaleta kila mtu ng'ombe wake pamoja naye usiku ule, nao wakawachinja hapo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawaambia, “Nendeni mkawaambie watu wote walete ng'ombe na kondoo wao hapa, wawachinje na kuwala hapa. Wasitende dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, kwa kula nyama yenye damu.” Hivyo, usiku ule wote walipeleka ng'ombe wao na kuwachinjia hapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Sauli akaagiza: Tawanyikeni katika watu na kuwaambia, kila mtu alete ng'ombe wake na mbuzi au kondoo wake huku kwangu, mwachinje hapa! Kisha mtawala pasipo kumkosea Bwana kwa kula damu. Ndipo, watu wote walipopeleka usiku huo kwa mikono yao kila mtu ng'ombe wake, wakawachinja hapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Sauli akasema, Haya! Tawanyikeni katikati ya watu mkawaambie, Nileteeni hapa kila mtu ng’ombe wake, na kila mtu kondoo wake, mkawachinje hapa na kula; wala msikose juu ya BWANA, kwa kula pamoja na damu. Nao watu wote wakaleta kila mtu ng’ombe wake pamoja naye usiku ule, nao wakawachinja hapo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaambia: “Muende muwaambie watu wote walete ngombe na kondoo wao hapa, wawachinje na kuwakula hapa. Wasitende zambi mbele ya Yawe, kwa kula nyama yenye damu.” Hivyo, usiku ule wote walipeleka ngombe wao na kuwachinjia pale.