1 Samuel 14:36 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Shauli akawaambia watu, “Twendeni tukawafuatie Wafilisti usiku, tukawavamie na kupora mali zao mpaka asubuhi; hatutamwacha mtu yeyote hai.” Watu wakamwambia, “Fanya unachoona kuwa chema kwako.” Lakini kuhani akawaambia, “Kwanza tuombe shauri kwa Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli akasema, “Tuteremke tufuatie Wafilisti usiku na kuwateka nyara hadi mapambazuko, nasi tusiache hata mmoja wao hai.” Wakajibu, “Fanya lolote lile uonalo jema zaidi kwako.” Lakini kuhani akasema, “Tuulize kwa Mungu mahali hapa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Sauli akasema, Haya! Na tushuke kuwafuata Wafilisti wakati wa usiku, na kuwateka nyara hata mapambazuko, wala tusiwaache hata mmoja wao. Nao wakamjibu, Fanya yo yote uyaonayo kuwa ni mema. Ndipo yule kuhani akasema, Na tumkaribie Mungu hapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Shauli akawaambia watu, “Twendeni tukawafuatie Wafilisti usiku, tukawavamie na kupora mali zao mpaka asubuhi; hatutamwacha mtu yeyote hai.” Watu wakamwambia, “Fanya unachoona kuwa chema kwako.” Lakini kuhani akawaambia, “Kwanza tuombe shauri kwa Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli akasema, “Tutelemke tufuatie Wafilisti usiku na kuwateka nyara mpaka mapambazuko, nasi tusiache hata mmoja wao hai.” Wakajibu, “Fanya lo lote lile uonalo jema zaidi kwako.” Lakini kuhani akasema, “Tuulize kwa Mungu mahali hapa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli akasema, “Tuteremke tufuatie Wafilisti usiku na kuwateka nyara mpaka mapambazuko, nasi tusiache hata mmoja wao hai.” Wakajibu, “Fanya lolote lile uonalo jema zaidi kwako.” Lakini kuhani akasema, “Tuulize kwa Mungu mahali hapa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Sauli akasema, Haya! Na tushuke kuwafuata Wafilisti wakati wa usiku, na kuwateka nyara hata mapambazuko, wala tusiwaache hata mmoja wao. Nao wakamjibu, Fanya lolote uonalo kuwa ni jema. Ndipo yule kuhani akasema, Na tumkaribie Mungu hapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Shauli akawaambia watu, “Twendeni tukawafuatie Wafilisti usiku, tukawavamie na kupora mali zao mpaka asubuhi; hatutamwacha mtu yeyote hai.” Watu wakamwambia, “Fanya unachoona kuwa chema kwako.” Lakini kuhani akawaambia, “Kwanza tuombe shauri kwa Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauli akasema: Na tutelemke kuwafukuza Wafilisti na usiku, tupate kuteka mateka kwao, mpaka kuche, tusisaze kwao mtu hata mmoja! Watu wakasema: Yote yaliyo mema machoni pako yafanye! Lakini mtambikaji akasema: Kwanza tumkaribie Mungu hapa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Sauli akasema, Haya! Na tushuke kuwafuata Wafilisti wakati wa usiku, na kuwateka nyara hata mapambazuko, wala tusiwaache hata mmoja wao. Nao wakamjibu, Fanya yo yote uyaonayo kuwa ni mema. Ndipo yule kuhani akasema, Na tumkaribie Mungu hapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Saulo akawaambia watu: “Twende tuwafuatilie Wafilistini usiku, tuwashambulie na kunyanganya mali zao mpaka asubui. Hatutamwacha mutu yeyote muzima.” Watu wakamwambia: “Fanya unachoona kuwa chema kwako.” Lakini kuhani akawaambia: “Kwanza tuombe shauri kwa Yawe.”