1 Samuel 14:41 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shauli akasema, “Ee Mwenyezi-Mungu wa Israeli, kwa nini hujanijibu mimi mtumishi wako? Ee Mwenyezi-Mungu wa Israeli, ikiwa hatia iko kwangu au kwa Yonathani mwanangu, basi, amua kwa jiwe la kauli ya Urimu. Lakini ikiwa hatia hiyo iko kwa watu wako wa Israeli, amua kwa jiwe la kauli ya Thumimu.” Yonathani na Shauli walipatikana kuwa na hatia, lakini watu walionekana hawana hatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Sauli akamwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, akisema, “Kwa nini hujamjibu mtumishi wako leo? Ikiwa makosa ni yangu au ya mwanangu Yonathani, jibu kwa Urimu. Lakini ikiwa makosa ni ya wanaume wa Israeli, jibu kwa Thumimu.” Yonathani na Sauli wakatolewa kwa kura, nao watu wakawa salama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo Sauli akamwambia Bwana, Mungu wa Israeli, [Kwani usimjibu mtumishi wako leo? Ikiwa dhambi i ndani yangu, au ndani yake Yonathani mwanangu, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, utoe Urimu; bali ukisema hivi, Dhambi i katika watu wako Israeli,]
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shauli akasema, “Ee Mwenyezi-Mungu wa Israeli, kwa nini hujanijibu mimi mtumishi wako? Ee Mwenyezi-Mungu wa Israeli, ikiwa hatia iko kwangu au kwa Yonathani mwanangu, basi, amua kwa jiwe la kauli ya Urimu. Lakini ikiwa hatia hiyo iko kwa watu wako wa Israeli, amua kwa jiwe la kauli ya Thumimu.” Yonathani na Shauli walipatikana kuwa na hatia, lakini watu walionekana hawana hatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Sauli akamwomba BWANA, Mungu wa Israeli, akisema, “Nipe jibu lililo sawa.” Yonathani na Sauli wakatolewa kwa kura, nao watu wakawa salama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Sauli akamwomba bwana, Mungu wa Israeli, akisema, “Nipe jibu lililo sawa.” Yonathani na Sauli wakatolewa kwa kura, nao watu wakawa salama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo Sauli akamwambia BWANA, Mungu wa Israeli, [Kwa nini usimjibu mtumishi wako leo? Ikiwa dhambi iko ndani yangu, au ndani yake Yonathani mwanangu, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, utoe Urimu; bali ukisema hivi, Dhambi iko katika watu wako Israeli,] utoe Thumimu. Basi Yonathani na Sauli wakatwaliwa, lakini watu wakapona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shauli akasema, “Ee Mwenyezi-Mungu wa Israeli, kwa nini hujanijibu mimi mtumishi wako? Ee Mwenyezi-Mungu wa Israeli, ikiwa hatia iko kwangu au kwa Yonathani mwanangu, basi, amua kwa jiwe la kauli ya Urimu. Lakini ikiwa hatia hiyo iko kwa watu wako wa Israeli, amua kwa jiwe la kauli ya Thumimu.” Yonathani na Shauli walipatikana kuwa na hatia, lakini watu walionekana hawana hatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Sauli akamwambia Bwana Mungu wa Isiraeli: Yaumbue yaliyokwisha kufanywa! Wakashikwa Yonatani na Sauli, nao watu wakapona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo Sauli akamwambia BWANA, Mungu wa Israeli, [Kwani usimjibu mtumishi wako leo? Ikiwa dhambi i ndani yangu, au ndani yake Yonathani mwanangu, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, utoe Urimu; bali ukisema hivi, Dhambi i katika watu wako Israeli,] utoe Thumimu. Basi Yonathani na Sauli wakatwaliwa, lakini watu wakapona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saulo akasema: “Ee Yawe wa Israeli, kwa nini haujanijibu mimi mutumishi wako? Ee Yawe wa Israeli, ikiwa kosa liko kwangu au kwa Yonatani mwana wangu, basi, jiwe la Urimu lionekane. Lakini ikiwa kosa hilo liko kwa watu wako Waisraeli, jiwe la Tumimu lionekane.” Yonatani na Saulo walipatikana kuwa na kosa, lakini watu walionekana hawana kosa.