1 Samuel 14:52 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulikuwa na mapigano makali dhidi ya Wafilisti muda wote Shauli alipokuwa mfalme; na kila mara Shauli alipompata mtu mwenye nguvu au shujaa alimchukua ajiunge na jeshi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku zote za utawala wa Sauli zilikuwa za vita vikali dhidi ya Wafilisti, na wakati wowote Sauli alimwona mtu mwenye nguvu au shujaa, alimchukua kwa utumishi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, kulikuwa na vita vikali sana juu ya Wafilisti siku zote za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu ye yote aliyekuwa hodari, au mtu ye yote aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulikuwa na mapigano makali dhidi ya Wafilisti muda wote Shauli alipokuwa mfalme; na kila mara Shauli alipompata mtu mwenye nguvu au shujaa alimchukua ajiunge na jeshi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku zote za kutawala kwa Sauli zilikuwa za vita vikali dhidi ya Wafilisti, na wakati wo wote Sauli alipomwona mtu mwenye nguvu au shujaa, alimchukua kwa utumishi wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku zote za utawala wa Sauli zilikuwa za vita vikali dhidi ya Wafilisti, na wakati wowote Sauli alimwona mtu mwenye nguvu au shujaa, alimchukua kwa utumishi wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, kulikuwa na vita kali sana juu ya Wafilisti siku zote za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu yeyote aliyekuwa hodari, au mtu yeyote aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulikuwa na mapigano makali dhidi ya Wafilisti muda wote Shauli alipokuwa mfalme; na kila mara Shauli alipompata mtu mwenye nguvu au shujaa alimchukua ajiunge na jeshi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vita vya kupigana na Wafilisti vikawa vikali siku zote za Sauli. Kwa hiyo kila mtu, Sauli aliyemwona kuwa fundi wa vita, na kila mtu mwenye nguvu akamchukua kuandamana naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, kulikuwa na vita vikali sana juu ya Wafilisti siku zote za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu ye yote aliyekuwa hodari, au mtu ye yote aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa vita kali na Wafilistini kwa muda wote Saulo alipokuwa mufalme. Na kila mara Saulo alipomupata mutu mwenye nguvu au shujaa alimukamata apate kujiunga na waaskari wake.