1 Samuel 14:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha, “Njoo, twende upande wa pili kwenye ile ngome ya hawa watu wasiotahiriwa. Huenda Mwenyezi-Mungu akatusaidia, maana Mwenyezi-Mungu haokoi kwa kutegemea wingi au uchache wa watu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yonathani akamwambia kijana wake mbeba silaha, “Njoo, tuvukie doria ya wale jamaa wasiotahiriwa. Huenda Mwenyezi Mungu atatenda kwa ajili yetu. Hakuna chochote kitakachoweza kumzuia Mwenyezi Mungu kuokoa, kwamba ni kwa wingi au kwa uchache.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na twende tukawavukie ngomeni hao wasiotahiriwa; yamkini Bwana atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia Bwana asiokoe, kwamba ni kwa wengi au kwamba ni kwa wachache.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha, “Njoo, twende upande wa pili kwenye ile ngome ya hawa watu wasiotahiriwa. Huenda Mwenyezi-Mungu akatusaidia, maana Mwenyezi-Mungu haokoi kwa kutegemea wingi au uchache wa watu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yonathani akamwambia kijana wake mbeba silaha, “Njoo, tuvukie doria ya wale jamaa wasiotahiriwa. Huenda BWANA atatenda kwa ajili yetu. Hakuna cho chote kitakachoweza kumzuia BWANA kuokoa, kwamba ni kwa wingi au kwa uchache.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yonathani akamwambia kijana wake mbeba silaha, “Njoo, tuvukie doria ya wale jamaa wasiotahiriwa. Huenda bwana atatenda kwa ajili yetu. Hakuna chochote kitakachoweza kumzuia bwana kuokoa, kwamba ni kwa wingi au kwa uchache.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha zake, Haya! Na twende tukavuke ngomeni mwa hao wasiotahiriwa; yamkini BWANA atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia BWANA asiokoe, kama ni kwa wengi au kama ni kwa wachache.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha, “Njoo, twende upande wa pili kwenye ile ngome ya hawa watu wasiotahiriwa. Huenda Mwenyezi-Mungu akatusaidia, maana Mwenyezi-Mungu haokoi kwa kutegemea wingi au uchache wa watu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yonatani akamwambia kijana aliyemchukulia mata: Haya! Twende, tuwavumbukie hao wamizimu wasiotahiriwa wanaongoja zamu! Labda Bwana atatupigania, kwani Bwana hashindwi na kuokoa, ikiwa anatumia wengi au wachache.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na twende tukawavukie ngomeni hao wasiotahiriwa; yamkini BWANA atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia BWANA asiokoe, kwamba ni kwa wengi au kwamba ni kwa wachache.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yonatani akamwambia yule kijana aliyemubebea silaha: “Kuja, tuende kwenye ile kambi ya hawa watu wasiotahiriwa. Labda Yawe atatusaidia, maana Yawe haokoi kwa kutegemea wingi au uchache wa watu.”