1 Samuel 15:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ninajuta kwamba nimemfanya Shauli kuwa mfalme. Yeye ameacha kunifuata mimi na hajatimiza amri zangu.” Samueli alikasirika, akamlilia Mwenyezi-Mungu usiku kucha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ninasikitika kwamba nimemfanya Sauli kuwa mfalme, kwa sababu ameacha kunifuata mimi na hakutimiza maagizo yangu.” Samweli akafadhaika, naye akamlilia Mwenyezi Mungu usiku ule wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ninajuta kwamba nimemfanya Shauli kuwa mfalme. Yeye ameacha kunifuata mimi na hajatimiza amri zangu.” Samueli alikasirika, akamlilia Mwenyezi-Mungu usiku kucha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ninasikitika kwamba nimemfanya Sauli kuwa mfalme, kwa sababu ameacha kunifuata mimi na hakutimiza maagizo yangu.” Samweli akafadhaika, naye akamlilia BWANA usiku ule wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ninasikitika kwamba nimemfanya Sauli kuwa mfalme, kwa sababu ameacha kunifuata mimi na hakutimiza maagizo yangu.” Samweli akafadhaika, naye akamlilia bwana usiku ule wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ninajuta kwamba nimemfanya Shauli kuwa mfalme. Yeye ameacha kunifuata mimi na hajatimiza amri zangu.” Samueli alikasirika, akamlilia Mwenyezi-Mungu usiku kucha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninaona majonzi, kwa kuwa nilimweka Sauli kuwa mfalme, kwani ameacha kunifuata, wala hayatimizi maneno yangu. Kwa hiyo moyo wake Samweli ukachafuka, akamlilia Bwana usiku wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ninajuta kwamba nimemufanya Saulo kuwa mufalme. Yeye ameacha kunifuata mimi na hajatimiza amri zangu.” Samweli alikasirika, akamulilia Yawe usiku kucha.