1 Samuel 15:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa sababu waliwapiga Waisraeli walipokuwa wanatoka Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa kile walichowatendea Israeli walipowavizia wakati walipanda kutoka Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa sababu waliwapiga Waisraeli walipokuwa wanatoka Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa kile walichowatendea Israeli walipowavizia wakati walipopanda kutoka Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa kile walichowatendea Israeli walipowavizia wakati walipanda kutoka Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu yale ambayo Waamaleki waliwatenda Waisraeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa sababu waliwapiga Waisraeli walipokuwa wanatoka Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Nitayalipiza, Waamaleki waliyowafanyizia Waisiraeli na kuwazibia njia, walipotoka Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi anasema hivi: ‘Nitawaazibu Waamaleki kwa ajili ya mambo waliyowatendea Waisraeli: wao waliwafungia njia walipokuwa wanatoka Misri.