1 Samuel 15:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Samueli akamwambia, “Je, Mwenyezi-Mungu anapendelea zaidi dhabihu za kuteketezwa na matambiko, kuliko kuitii sauti yake? Tazama, kumtii yeye ni bora kuliko matambiko na kumsikiliza kuliko kumtambikia mafuta ya beberu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Samweli akajibu: “Je, Mwenyezi Mungu anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu kama vile kuitii sauti ya Mwenyezi Mungu? Kutii ni bora kuliko dhabihu, nako kusikia ni bora kuliko mafuta ya kondoo dume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Samueli akamwambia, “Je, Mwenyezi-Mungu anapendelea zaidi dhabihu za kuteketezwa na matambiko, kuliko kuitii sauti yake? Tazama, kumtii yeye ni bora kuliko matambiko na kumsikiliza kuliko kumtambikia mafuta ya beberu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Samweli akajibu: “Je, BWANA anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu kama vile kuitii sauti ya BWANA? Kutii ni bora zaidi kuliko dhabihu, nako kusikia ni bora kuliko mafuta ya kondoo dume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Samweli akajibu: “Je, bwana anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu kama vile kuitii sauti ya bwana? Kutii ni bora zaidi kuliko dhabihu, nako kusikia ni bora kuliko mafuta ya kondoo dume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Samweli akasema, Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikiliza ushauri kuliko mafuta ya beberu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Samueli akamwambia, “Je, Mwenyezi-Mungu anapendelea zaidi dhabihu za kuteketezwa na matambiko, kuliko kuitii sauti yake? Tazama, kumtii yeye ni bora kuliko matambiko na kumsikiliza kuliko kumtambikia mafuta ya beberu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Samweli akamwambia: Je? Bwana anapendezwa na vipaji vya tambiko, ijapo ziwe ng'ombe za kuteketezwa nzima, kama anavyopendezwa ukikiitikia kinywa chake Bwana? Tazama, kutii ni kwema kuliko vipaji vya tambiko, nako kusikiliza ni kwema kuliko mafuta ya kondoo;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Samweli akamwambia: “Unazani kwamba Yawe anapendelea zaidi sadaka za kuteketezwa kwa moto na matoleo mengine, kuliko kuitii sauti yake? Hapana. Kumutii yeye ni bora kuliko matoleo na kumusikiliza kuliko kumutolea mafuta ya beberu.