1 Samuel 15:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uasi ni sawa na dhambi ya kupiga ramli, na kiburi ni sawa na uovu na kuabudu vinyago. Kwa sababu umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu, naye amekukataa kuwa mfalme.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi, nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu. Kwa sababu umelikataa neno la Mwenyezi Mungu, naye amekukataa wewe kuendelea kuwa mfalme.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uasi ni sawa na dhambi ya kupiga ramli, na kiburi ni sawa na uovu na kuabudu vinyago. Kwa sababu umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu, naye amekukataa kuwa mfalme.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi, nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu. Kwa sababu umelikataa neno la BWANA, naye amekukataa wewe kuendelea kuwa mfalme.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi, nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu. Kwa sababu umelikataa neno la bwana, naye amekukataa wewe kuendelea kuwa mfalme.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama uovu na kuabudu vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Uasi ni sawa na dhambi ya kupiga ramli, na kiburi ni sawa na uovu na kuabudu vinyago. Kwa sababu umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu, naye amekukataa kuwa mfalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani upingani ni ukosaji sawasawa kama uchawi, nao ubishi ni upotovu kama kutambikia mizimu. Kwa kuwa umelitangua neno lake Bwana, naye amekutangua, usiwe mfalme tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uasi ni sawa na zambi ya kuaguza, na kiburi ni sawa na uovu wa kuabudu sanamu. Kwa sababu umeikataa amri ya Yawe, naye amekukataa kuwa mufalme.”