1 Samuel 15:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, nenda ukawashambulie na kuangamiza vitu vyote walivyo navyo. Usiwaache hai, ila uwaue wote: Wanaume kwa wanawake, watoto wachanga na wanyonyao, ng'ombe, kondoo, ngamia na punda.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie; waue wanaume na wanawake, watoto na wale wanaonyonya, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, nenda ukawashambulie na kuangamiza vitu vyote walivyo navyo. Usiwaache hai, ila uwaue wote: wanaume kwa wanawake, watoto wachanga na wanyonyao, ng'ombe, kondoo, ngamia na punda.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie, waue wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie; waue wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, nenda ukawashambulie na kuangamiza vitu vyote walivyo navyo. Usiwaache hai, ila uwaue wote: Wanaume kwa wanawake, watoto wachanga na wanyonyao, ng'ombe, kondoo, ngamia na punda.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa nenda, uwapige Waamaleki! Lakini vyote pia, walivyo navyo, sharti viwe mwiko kwenu wa kuwapo, msivionee uchungu, ila sharti mwaue waume hata wake, watoto hata wachanga, ng'ombe hata kondoo, ngamia hata punda!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, uende kushambulia na kuangamiza vitu vyote wanavyokuwa navyo. Usiwaache wazima, lakini uwaue wote: wanaume kwa wanawake, watoto wachanga na wenye kunyonya, ngombe, kondoo, ngamia na punda.’ ”