1 Samuel 15:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shauli akajibu, “Nimefanya dhambi. Hata hivyo, unistahi sasa mbele ya wazee wa watu wangu na Waisraeli. Niruhusu nirudi pamoja nawe ili nikamwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli akajibu, “Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali niheshimu mbele ya wazee wa watu wangu na mbele ya Israeli; rudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu Bwana, Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shauli akajibu, “Nimefanya dhambi. Hata hivyo, unistahi sasa mbele ya wazee wa watu wangu na Waisraeli. Niruhusu nirudi pamoja nawe ili nikamwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli akajibu, “Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali niheshimu mbele ya wazee wa watu wangu na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu BWANA Mungu wako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli akajibu, “Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali niheshimu mbele ya wazee wa watu wangu na mbele ya Israeli; rudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu bwana Mwenyezi Mungu wako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu BWANA, Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shauli akajibu, “Nimefanya dhambi. Hata hivyo, unistahi sasa mbele ya wazee wa watu wangu na Waisraeli. Niruhusu nirudi pamoja nawe ili nikamwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauli akasema: Nimekosa kweli, lakini sasa unipe macheo kwenye hawa wazee wao walio ukoo wangu nako kwao Waisiraeli ukirudi pamoja nami, nije kumwangukia Bwana Mungu wako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu BWANA, Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saulo akajibu: “Nimefanya zambi. Hata hivyo, uniheshimishe sasa mbele ya wazee wa watu wangu na Waisraeli. Uniruhusu nirudi pamoja nawe kusudi nimwabudu Yawe, Mungu wako.”