1 Samuel 15:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Shauli na watu wake hawakumuua Agagi, wala kondoo bora kabisa, ng'ombe wazuri, ndama, wanakondoo na chochote kile kilichokuwa kizuri hawakukiangamiza. Lakini vitu vyote vibaya na visivyo na thamani waliviangamiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi, na kondoo na ng’ombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona, na kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Shauli na watu wake hawakumuua Agagi, wala kondoo bora kabisa, ng'ombe wazuri, ndama, wanakondoo na chochote kile kilichokuwa kizuri hawakukiangamiza. Lakini vitu vyote vibaya na visivyo na thamani waliviangamiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi na kondoo na ng'ombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi na kondoo na ng’ombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Shauli na watu wake hawakumuua Agagi, wala kondoo bora kabisa, ng'ombe wazuri, ndama, wanakondoo na chochote kile kilichokuwa kizuri hawakukiangamiza. Lakini vitu vyote vibaya na visivyo na thamani waliviangamiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Sauli pamoja na watu wake wakamhurumia Agagi na mbuzi na kondoo na ng'ombe waliokuwa wazuri kwa kunona na wana kondoo na nyama wengine wa kufuga waliokuwa wazuri, hawakutaka kuwatia mwiko wa kuwapo, wawaue; lakini nyama wote waliokuwa wabayabaya kwa kuugua, ndio, waliowatia mwiko wa kuwapo, wakawaua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Saulo na watu wake hawakumwua Agagi, kondoo bora kabisa, ngombe wazuri, wana-ngombe, wana-kondoo na chochote kile kilichokuwa kizuri hawakukiangamiza. Lakini vitu vyote vibaya na visivyokuwa vya bei kali waliviangamiza.