1 Samuel 16:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, Yese alituma mtu, naye akaletwa. Yule kijana alikuwa mwenye afya, mwenye macho maangavu na wa kupendeza. Mwenyezi-Mungu akamwambia Samueli, “Sasa, huyu ndiye; inuka umpake mafuta.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi akatuma aitwe, naye akaletwa. Aling’aa kwa afya, na mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza. Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, “Inuka na umpake mafuta; huyu ndiye.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, Yese alituma mtu, naye akaletwa. Yule kijana alikuwa mwenye afya, mwenye macho maangavu na wa kupendeza. Mwenyezi-Mungu akamwambia Samueli, “Sasa, huyu ndiye; inuka umpake mafuta.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza. Ndipo BWANA akasema, “Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza. Ndipo bwana akasema, “Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. BWANA akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, Yese alituma mtu, naye akaletwa. Yule kijana alikuwa mwenye afya, mwenye macho maangavu na wa kupendeza. Mwenyezi-Mungu akamwambia Samueli, “Sasa, huyu ndiye; inuka umpake mafuta.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, akatuma, wakamleta, naye alikuwa mwekundu mwenye macho mazuri na umbo jema. Ndipo, Bwana alipomwambia: Haya! Umpake mafuta! Kwani huyu ndiye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. BWANA akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo, Yese alituma mutu, naye akaletwa. Yule kijana alikuwa mwenye afya, mwenye macho yenye kungaa na wa kupendeza. Yawe akamwambia Samweli: “Sasa, huyu ndiye; simama umupakae mafuta.”