1 Samuel 16:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Samueli akasema, “Nitawezaje kwenda? Kama Shauli akisikia habari hizo, ataniua!” Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Chukua ndama pamoja nawe, na ukifika huko useme, ‘Nimekuja kumtolea Mwenyezi-Mungu tambiko’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Samweli akasema, “Nitaendaje? Sauli atasikia kuhusu jambo hili na ataniua.” Mwenyezi Mungu akamwambia, “Chukua ndama jike, useme, ‘Nimekuja kumtolea Mwenyezi Mungu dhabihu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Samueli akasema, “Nitawezaje kwenda? Kama Shauli akisikia habari hizo, ataniua!” Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Chukua ndama pamoja nawe, na ukifika huko useme, ‘Nimekuja kumtolea Mwenyezi-Mungu tambiko’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Samweli akasema, “Nitakwendaje? Sauli atasikia juu ya jambo hili na ataniua.” BWANA akamwambia, “Chukua mtamba wa ng'ombe na useme, ‘Nimekuja kumtolea BWANA dhabihu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Samweli akasema, “Nitakwendaje? Sauli atasikia juu ya jambo hili na ataniua.” bwana akamwambia, “Chukua mtamba wa ng’ombe na useme, ‘Nimekuja kumtolea bwana dhabihu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi BWANA akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea BWANA dhabihu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Samueli akasema, “Nitawezaje kwenda? Kama Shauli akisikia habari hizo, ataniua!” Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Chukua ndama pamoja nawe, na ukifika huko useme, ‘Nimekuja kumtolea Mwenyezi-Mungu tambiko’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Samweli akasema: Nitakwendaje? Sauli akivisikia ataniua. Bwana akasema: Chukua mori ya ng'ombe mkononi mwako, useme: Nimekuja kumtambikia Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi BWANA akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea BWANA dhabihu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Samweli akasema: “Nitaweza kwenda namna gani? Kama Saulo akisikia habari hiyo, ataniua!” Yawe akamwambia: “Twaa mwana-ngombe pamoja nawe, na ukifika kule useme: ‘Nimekuja kumutolea Yawe sadaka’.