1 Samuel 16:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mara, yule roho mwovu kutoka kwa Mungu alipomjia Shauli, Daudi alichukua kinubi chake na kuanza kukipiga, na roho huyo alimwacha Shauli, naye akaburudika na kupata nafuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mara roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ilipomjia Sauli, Daudi alichukua kinubi chake na kupiga. Ndipo Sauli angetulizwa na kujisikia vizuri, nayo ile roho mbaya ingemwacha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mara, yule roho mwovu kutoka kwa Mungu alipomjia Shauli, Daudi alichukua kinubi chake na kuanza kukipiga, na roho huyo alimwacha Shauli, naye akaburudika na kupata nafuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mara roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ilipomjia Sauli, Daudi alichukua kinubi chake na kupiga. Ndipo Sauli angetulizwa na kujisikia vizuri, nayo ile roho mbaya ingemwacha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mara roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ilipomjia Sauli, Daudi alichukua kinubi chake na kupiga. Ndipo Sauli angetulizwa na kujisikia vizuri, nayo ile roho mbaya ingemwacha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjia Sauli, ndipo Daudi alipokishika kinubi na kukipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mara, yule roho mwovu kutoka kwa Mungu alipomjia Shauli, Daudi alichukua kinubi chake na kuanza kukipiga, na roho huyo alimwacha Shauli, naye akaburudika na kupata nafuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa kila mara, ile roho ya Mungu ilipomjia Sauli, Dawidi akalichukua zeze lake, akalipiga kwa mkono wake; ndipo, Sauli alipotulia na kuona vema, ile roho mbaya ikaondoka kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mara, yule roho mwovu kutoka kwa Mungu alipomufikia Saulo, Daudi alitwaa kinubi chake na kuanza kukipiga, na roho yule alimwacha Saulo, naye akajisikia vizuri na kupata utulivu.