1 Samuel 16:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Samueli akafanya kama alivyoambiwa na Mwenyezi-Mungu, akaenda Bethlehemu. Wazee wa mji wakatoka kumlaki wakiwa wanatetemeka, wakamwuliza, “Je, umekuja kwa amani?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Samweli akafanya kile Mwenyezi Mungu alichosema. Alipofika Bethlehemu, wazee wa mji wakatetemeka walipomlaki. Wakauliza, “Je, umekuja kwa amani?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Samweli akafanya hayo aliyosema Bwana, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Samueli akafanya kama alivyoambiwa na Mwenyezi-Mungu, akaenda Bethlehemu. Wazee wa mji wakatoka kumlaki wakiwa wanatetemeka, wakamwuliza, “Je, umekuja kwa amani?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Samweli akafanya kile BWANA alichosema. Alipofika Bethlehemu, wazee wa mji wakatetemeka walipomlaki. Wakauliza, “Je, umekuja kwa amani?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Samweli akafanya kile bwana alichosema. Alipofika Bethlehemu, wazee wa mji wakatetemeka walipomlaki. Wakauliza, “Je, umekuja kwa amani?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Samweli akafanya hayo aliyosema BWANA, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Samueli akafanya kama alivyoambiwa na Mwenyezi-Mungu, akaenda Bethlehemu. Wazee wa mji wakatoka kumlaki wakiwa wanatetemeka, wakamwuliza, “Je, umekuja kwa amani?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Samweli akayafanya, Bwana aliyomwambia. Alipofika Beti-Lehemu, wazee wa mji wakamjia njiani na kutetemeka, wakamwamkia kwamba: Kuja kwako ni kwema?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Samweli akafanya hayo aliyosema BWANA, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Samweli akafanya sawa alivyoambiwa na Yawe, akaenda Betelehemu. Wazee wa muji wakatoka kwenda kumupokea wakiwa wanatetemeka, wakamwuliza: “Umekuja kwa amani?”