1 Samuel 17:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akawauliza wale waliokuwa karibu naye, “Je, mtu atakayemuua Mfilisti huyu na kuikomboa Israeli kutokana na aibu hii atafanyiwa nini? Ni nani huyu Mfilisti, mtu asiyetahiriwa, anayethubutu kuyatukana majeshi ya Mungu aliye hai?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akauliza watu waliokuwa wamesimama karibu naye, “Je, atatendewa nini mtu atakayemuua huyu Mfilisti na kuondoa aibu hii katika Israeli? Ni nani huyu Mfilisti asiyetahiriwa hata atukane majeshi ya Mungu aliye hai?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akawauliza wale waliokuwa karibu naye, “Je, mtu atakayemuua Mfilisti huyu na kuikomboa Israeli kutokana na aibu hii atafanyiwa nini? Ni nani huyu Mfilisti, mtu asiyetahiriwa, anayethubutu kuyatukana majeshi ya Mungu aliye hai?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akauliza watu waliokuwa wamesimama karibu naye, “Je, atafanyiwa nini mtu atakayemwua huyu Mfilisti na kuondoa aibu hii itoke katika Israeli? Ni nani huyu Mfilisti asiyetahiriwa hata atukane majeshi ya Mungu aliye hai?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akauliza watu waliokuwa wamesimama karibu naye, “Je, atafanyiwa nini mtu atakayemuua huyu Mfilisti na kuondoa aibu hii katika Israeli? Ni nani huyu Mfilisti asiyetahiriwa hata atukane majeshi ya Mungu aliye hai?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akawauliza wale waliokuwa karibu naye, “Je, mtu atakayemuua Mfilisti huyu na kuikomboa Israeli kutokana na aibu hii atafanyiwa nini? Ni nani huyu Mfilisti, mtu asiyetahiriwa, anayethubutu kuyatukana majeshi ya Mungu aliye hai?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akawauliza wale watu waliosimama pamoja naye akisema: Mtu akimpiga huyo Mfilisti na kuiondoa soni kwao Waisiraeli atafanyiziwa nini? Kwani huyo Mfilisti asiyetahiriwa ni mtu gani akiwatweza wapiga vita wa Mungu aliye Mwenye uzima?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akawauliza wale waliokuwa karibu naye: “Mutu atakayemwua Mufilistini huyu na kuikomboa Israeli kutokana na haya hii atafanyiwa nini? Ni nani huyu Mufilistini, mutu mupagani, anayesubutu kuwatukana waaskari wa Mungu Mwenye Uzima?”