1 Samuel 17:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akamwambia Shauli, “Mtu yeyote asitishike moyoni mwake kutokana na Mfilisti huyu. Mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana naye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akamwambia Sauli, “Mtu yeyote asife moyo kwa habari ya huyu Mfilisti; mtumishi wako ataenda kupigana naye.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akamwambia Shauli, “Mtu yeyote asitishike moyoni mwake kutokana na Mfilisti huyu. Mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana naye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akamwambia Sauli, “Mtu ye yote asife moyo kwa habari ya huyu Mfilisti; mtumishi wako atakwenda kupigana naye.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akamwambia Sauli, “Mtu yeyote asife moyo kwa habari ya huyu Mfilisti; mtumishi wako atakwenda kupigana naye.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi akamwambia Sauli, Asifadhaike moyo mtu yeyote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akamwambia Shauli, “Mtu yeyote asitishike moyoni mwake kutokana na Mfilisti huyu. Mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana naye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akamwambia Sauli: Mtu asipotelewe na moyo kwa ajili yake yeye! Mtoto wako atakwenda kupigana na huyo Mfilisti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamwambia Saulo: “Mutu yeyote asitishike ndani ya moyo wake kutokana na Mufilistini huyu. Mimi mutumishi wako nitakwenda kupigana naye.”