1 Samuel 17:45 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Daudi akamwambia Goliathi, “Wewe unanijia kwa upanga, mkuki na sime. Lakini mimi ninakujia kwa jina la Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa askari wa Israeli, ambaye wewe umemtukana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akamwambia yule Mfilisti. “Wewe unanijia na upanga, mkuki na fumo, lakini mimi ninakujia kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa majeshi ya Israeli, ambaye wewe umemtukana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Daudi akamwambia Goliathi, “Wewe unanijia kwa upanga, mkuki na sime. Lakini mimi ninakujia kwa jina la Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa askari wa Israeli, ambaye wewe umemtukana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akamwambia yule Mfilisti. “Wewe unanijia na upanga, mkuki na fumo, lakini mimi ninakujia kwa jina la BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa majeshi ya Israeli, ambaye wewe umemtukana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akamwambia yule Mfilisti. “Wewe unanijia na upanga, mkuki na fumo, lakini mimi ninakujia kwa jina la bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa majeshi ya Israeli, ambaye wewe umemtukana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Daudi akamwambia Goliathi, “Wewe unanijia kwa upanga, mkuki na sime. Lakini mimi ninakujia kwa jina la Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa askari wa Israeli, ambaye wewe umemtukana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Dawidi akamwambia Mfilisti: Wewe unanijia na kushika upanga na mkuki na ngao, lakini mimi ninakujia katika Jina la Bwana Mwenye vikosi, aliye Mungu wao wapiga vita vya Waisiraeli, uliyemtukana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Daudi akamwambia Goliati: “Wewe unanifikia kwa upanga na mikuki. Lakini mimi ninakufikia kwa jina la Yawe wa majeshi, Mungu wa waaskari wa Israeli, ambaye wewe umemutukana.