1 Samuel 17:52 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo watu wa Israeli na watu wa Yuda, walipoanza kupiga kelele za ushindi, wakawafuatilia Wafilisti hadi Gathi, kwenye malango ya Ekroni, hata Wafilisti waliojeruhiwa vitani walienea njiani tangu Shaarimu hadi Gathi na Ekroni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wanaume wa Israeli na Yuda wakainuka kwenda mbele wakipiga kelele na kufuatia Wafilisti hadi kwenye ingilio la Gathi kwenye malango ya Ekroni. Maiti zao zilitawanyika kando ya barabara ya Shaaraimu hadi Gathi na Ekroni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watu wa Israeli na wa Yuda wakainuka, na kupiga kelele, nao wakawafuata Wafilisti mpaka ufikapo Gathi, na mpaka malango ya Ekroni. Nao majeruhi wa Wafilisti wakaanguka kando ya njia iendayo Shaarimu, mpaka Gathi, na mpaka Ekroni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo watu wa Israeli na watu wa Yuda, walipoanza kupiga kelele za ushindi, wakawafuatilia Wafilisti hadi Gathi, kwenye malango ya Ekroni, hata Wafilisti waliojeruhiwa vitani walienea njiani tangu Shaarimu hadi Gathi na Ekroni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo watu wa Israeli na Yuda wakainuka kwenda mbele wakipiga kelele na kufuatia Wafilisti mpaka kwenye ingilio la Gathi kwenye malango ya Ekroni. Maiti zao zilitawanyika kando ya barabara ya Shaaraimu hadi Gathi na Ekroni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo watu wa Israeli na Yuda wakainuka kwenda mbele wakipiga kelele na kufuatia Wafilisti mpaka kwenye ingilio la Gathi kwenye malango ya Ekroni. Maiti zao zilitawanyika kando ya barabara ya Shaaraimu hadi Gathi na Ekroni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watu wa Israeli na wa Yuda wakainuka, na kupiga kelele, nao wakawafuata Wafilisti mpaka Gathi, na mpaka malango ya Ekroni. Nao majeruhi wa Wafilisti wakaanguka kando ya njia iendayo Shaarimu, mpaka Gathi, na mpaka Ekroni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo watu wa Israeli na watu wa Yuda, walipoanza kupiga kelele za ushindi, wakawafuatilia Wafilisti hadi Gathi, kwenye malango ya Ekroni, hata Wafilisti waliojeruhiwa vitani walienea njiani tangu Shaarimu hadi Gathi na Ekroni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watu wa Waisiraeli na Wayuda wakainuka, wakaondoka na kupiga yowe, wakawakimbiza Wafilisti mpaka kufika Gai na malango ya Ekroni, nao Wafilisti walioumizwa wakaanguka njiani kwenda Saraimu, hata Gati na Ekroni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watu wa Israeli na wa Yuda wakainuka, na kupiga kelele, nao wakawafuata Wafilisti mpaka ufikapo Gathi, na mpaka malango ya Ekroni. Nao majeruhi wa Wafilisti wakaanguka kando ya njia iendayo Shaarimu, mpaka Gathi, na mpaka Ekroni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu watu wa Israeli na watu wa Yuda walianza kupiga kelele za ushindi, wakawafuatilia Wafilistini mpaka Gati, kwenye milango ya muji wa Ekroni, hata Wafilistini walioumizwa katika vita walikufa katika njia tangu Saraimu mpaka Gati na Ekroni.