1 Samuel 17:55 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shauli alipomwona Daudi akienda kumkabili yule Mfilisti Goliathi, alimwuliza Abneri, kamanda wa jeshi lake, “Abneri, huyu ni kijana wa nani?” Abneri alijibu, “Mfalme, kama uishivyo, mimi sijui.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli alipomwona Daudi anaenda kukabiliana na huyo Mfilisti, alimwambia Abneri, jemadari wa jeshi, “Abneri, yule kijana ni mwana wa nani?” Abneri akajibu, “Hakika kama uishivyo, ee mfalme, mimi sifahamu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Sauli, hapo alipomwona Daudi akitoka ili kumwendea yule Mfilisti, alimwambia Abneri, jemadari wa jeshi, Je! Abneri, kijana huyu ni mwana wa nani? Abneri akamjibu, Ee mfalme, kama iishivyo roho yako, mimi siwezi kusema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shauli alipomwona Daudi akienda kumkabili yule Mfilisti Goliathi, alimwuliza Abneri, kamanda wa jeshi lake, “Abneri, huyu ni kijana wa nani?” Abneri alijibu, “Mfalme, kama uishivyo, mimi sijui.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Sauli alipomwona Daudi anakwenda kukabiliana na huyo Mfilisti, alimwambia Abneri, jemadari wa jeshi, “Abneri, yule kijana ni mwana wa nani?” Abneri akajibu, “Hakika kama uishivyo, Ee mfalme, mimi sifahamu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli alipomwona Daudi anakwenda kukabiliana na huyo Mfilisti, alimwambia Abneri, jemadari wa jeshi, “Abneri, yule kijana ni mwana wa nani?” Abneri akajibu, “Hakika kama uishivyo, ee mfalme, mimi sifahamu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sauli alipomwona Daudi akitoka ili kumwendea yule Mfilisti, alimwambia Abneri, jemadari wa jeshi, Je! Abneri, kijana huyu ni mwana wa nani? Abneri akamjibu, Ee mfalme, kama iishivyo roho yako, mimi sijui.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shauli alipomwona Daudi akienda kumkabili yule Mfilisti Goliathi, alimwuliza Abneri, kamanda wa jeshi lake, “Abneri, huyu ni kijana wa nani?” Abneri alijibu, “Mfalme, kama uishivyo, mimi sijui.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauli alipoona, Dawidi alivyotoka, akutane na yule Mfilisti, akamwuliza Abineri, mkuu wa vikosi: Huyu kijana ni mwana wa nani? Abineri akasema: Hivyo roho yako, mfalme, ilivyo nzima, sijui.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Sauli, hapo alipomwona Daudi akitoka ili kumwendea yule Mfilisti, alimwambia Abneri, jemadari wa jeshi, Je! Abneri, kijana huyu ni mwana wa nani? Abneri akamjibu, Ee mfalme, kama iishivyo roho yako, mimi siwezi kusema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saulo alipomwona Daudi akienda kupigana na yule Mufilistini Goliati, alimwuliza Abeneri, jemadari wa kundi lake: “Abeneri, huyu ni kijana wa nani?” Abeneri alijibu: “Ee Mufalme, ninaapa kwa jina lako, mimi sijui.”