1 Samuel 17:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Goliathi alisimama na kuwapigia kelele wanajeshi wa Israeli, akisema, “Mnafanya nini hapo? Je, mmekuja kupigana vita? Mimi ni Mfilisti, nyinyi ni watumwa wa Shauli. Chagueni mtu mmoja wenu aje kupigana nami.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Goliathi alisimama na kuwaambia majeshi ya Israeli kwa sauti kuu, akisema, “Kwa nini mmetoka kupanga vita? Je, mimi si Mfilisti, na ninyi ni watumishi wa Sauli? Chagueni mtu na anishukie mimi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Goliathi alisimama na kuwapigia kelele wanajeshi wa Israeli, akisema, “Mnafanya nini hapo? Je, mmekuja kupigana vita? Mimi ni Mfilisti, nyinyi ni watumwa wa Shauli. Chagueni mtu mmoja wenu aje kupigana nami.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Goliathi alisimama na kuwapigia kelele majeshi ya Israeli, akisema, “Kwa nini mmetoka kupanga vita? Je, mimi si Mfilisti, na ninyi ni watumishi wa Sauli? Chagueni mtu na anishukie mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Goliathi alisimama na kuwapigia kelele majeshi ya Israeli, akisema, “Kwa nini mmetoka kupanga vita? Je, mimi si Mfilisti, na ninyi ni watumishi wa Sauli? Chagueni mtu na anishukie mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Goliathi alisimama na kuwapigia kelele wanajeshi wa Israeli, akisema, “Mnafanya nini hapo? Je, mmekuja kupigana vita? Mimi ni Mfilisti, nyinyi ni watumwa wa Shauli. Chagueni mtu mmoja wenu aje kupigana nami.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaja kusimama mbele akipaza sauti sana na kuwaita Waisiraeli waliojipanga, akawaambia: Mbona mmetoka, mkajipanga kupiga vita? Mimi si Mfilisti? Nanyi sio watu wa Sauli? Chagueni mtu wa kwenu, ashuke kuja kwangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akasimama, akawapigia kelele majeshi ya Israeli akawaambia, Mbona mmetoka kupanga vita? Je! Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Jichagulieni mtu, akanishukie mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Goliati alisimama na kuwapigia kelele waaskari wa Waisraeli, akisema: “Munafanya nini pale? Mumekuja kupigana vita? Mimi ni Mufilistini; ninyi ni watumwa wa Saulo. Muchague mutu mumoja kati yenu akuje kupigana nami.