1 Samuel 18:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake, roho mwovu kutoka kwa Mungu, alimvamia Shauli kwa ghafla, akawa anapayukapayuka kama mwendawazimu nyumbani kwake. Daudi alikuwa anapiga kinubi kama alivyofanya siku zote. Shauli alikuwa na mkuki mkononi mwake;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kesho yake roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ikaja kwa nguvu juu ya Sauli. Alikuwa akitabiri nyumbani mwake, wakati Daudi alikuwa akipiga kinubi, kama alivyozoea. Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake, roho mwovu kutoka kwa Mungu, alimvamia Shauli kwa ghafla, akawa anapayukapayuka kama mwendawazimu nyumbani kwake. Daudi alikuwa anapiga kinubi kama alivyofanya siku zote. Shauli alikuwa na mkuki mkononi mwake;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kesho yake roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ikaja kwa nguvu juu ya Sauli. Alikuwa akitabiri nyumbani mwake, wakati Daudi alipokuwa akipiga kinubi, kama alivyozoea. Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kesho yake roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ikaja kwa nguvu juu ya Sauli. Alikuwa akitabiri nyumbani mwake, wakati Daudi alikuwa akipiga kinubi, kama alivyozoea. Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake, roho mwovu kutoka kwa Mungu, alimvamia Shauli kwa ghafla, akawa anapayukapayuka kama mwendawazimu nyumbani kwake. Daudi alikuwa anapiga kinubi kama alivyofanya siku zote. Shauli alikuwa na mkuki mkononi mwake;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake ile roho mbaya ya Mungu ikampagaa Sauli, akawa nyumbani mwake kama mwenye wazimu akipayukapayuka, lakini Dawidi akampigia zeze kwa mkono wake, kama alivyozoea siku zote, naye Sauli akawa akishika mkuki mkononi mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake, pepo muchafu kutoka kwa Mungu akamushambulia Saulo kwa rafla, akakuwa anapayukapayuka kama mwenda-wazimu katika nyumba yake. Daudi alikuwa anapiga kinubi kama alivyofanya siku zote. Saulo alikuwa na mukuki katika mukono wake.