1 Samuel 18:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shauli akawaambia, “Mwambieni Daudi hivi: ‘Kile ambacho mfalme anataka kama mahari ya binti yake ni magovi 100 ya Wafilisti, ili ajilipize kisasi cha adui zake.’” [Hivi ndivyo Shauli alivyopanga Daudi auawe na Wafilisti.]
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli akajibu, “Mwambieni Daudi, ‘Mfalme hataki zawadi nyingine kuwa mahari, isipokuwa magovi mia moja ya Wafilisti, ili kulipiza kisasi juu ya adui zake.’ ” Mawazo ya Sauli yalikuwa Daudi akaanguke mikononi mwa Wafilisti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Sauli akasema, Mwambieni Daudi hivi, Mfalme hataki mahari yo yote, ila anataka govi mia za Wafilisti, ili ajilipize kisasi adui za mfalme. Basi Sauli alidhani kumwangamiza Daudi kwa mkono wa Wafilisti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shauli akawaambia, “Mwambieni Daudi hivi: ‘Kile ambacho mfalme anataka kama mahari ya binti yake ni magovi 100 ya Wafilisti, ili ajilipize kisasi cha adui zake.’” [Hivi ndivyo Shauli alivyopanga Daudi auawe na Wafilisti.]
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli akajibu, “Mwambieni Daudi, ‘Mfalme hataki zawadi nyingine kuwa mahari isipokuwa magovi 100 ya Wafilisti, ili kulipiza kisasi juu ya adui zake.’ ” Mawazo ya Sauli yalikuwa Daudi akaanguke mikononi mwa Wafilisti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli akajibu, “Mwambieni Daudi, ‘Mfalme hataki zawadi nyingine kuwa mahari isipokuwa magovi 100 ya Wafilisti, ili kulipiza kisasi juu ya adui zake.’ ” Mawazo ya Sauli yalikuwa Daudi akaanguke mikononi mwa Wafilisti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Sauli akasema, Mwambieni Daudi hivi, Mfalme hataki mahari yoyote, ila anataka govi mia moja za Wafilisti, ili ajilipize kisasi adui za mfalme. Basi Sauli alidhani kumwangamiza Daudi kwa mkono wa Wafilisti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shauli akawaambia, “Mwambieni Daudi hivi: ‘Kile ambacho mfalme anataka kama mahari ya binti yake ni magovi 100 ya Wafilisti, ili ajilipize kisasi cha adui zake.’” [Hivi ndivyo Shauli alivyopanga Daudi auawe na Wafilisti.]
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Sauli aliposema: Mwambieni Dawidi haya: mfalme hataki mali nyingine za ukwe, anataka tu magovi mia za Wafilisti, ajilipize kwao hao adui za mfalme. Lakini Sauli alifikiri moyoni njia ya kumtia Dawidi mikononi mwa Wafilisti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Sauli akasema, Mwambieni Daudi hivi, Mfalme hataki mahari yo yote, ila anataka govi mia za Wafilisti, ili ajilipize kisasi adui za mfalme. Basi Sauli alidhani kumwangamiza Daudi kwa mkono wa Wafilisti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saulo akawaambia: “Mumwambie Daudi hivi: ‘Kile ambacho mufalme anataka kama vile mali kwa binti yake ni magovi mia moja ya Wafilistini, kusudi ajilipize kisasi kwa waadui zake.’ ” Hivi ndivyo Saulo alivyopanga kusudi Daudi auawe na Wafilistini.