1 Samuel 19:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shauli alijaribu kumchoma Daudi kwa mkuki huo, Lakini Daudi alikwepa mkuki wa Shauli na mkuki ukapiga ukuta. Daudi akakimbia na kutoroka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli akajaribu kumchomea Daudi ukutani kwa huo mkuki wake, lakini Daudi akauhepa huo mkuki wa Sauli ukakita ukutani. Usiku ule ule Daudi akakimbia na kuokoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sauli akajaribu kumpiga Daudi hata ukutani kwa mkuki wake, ila yeye akaponyoka kutoka mbele ya Sauli, nao huo mkuki akaupiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shauli alijaribu kumchoma Daudi kwa mkuki huo, Lakini Daudi alikwepa mkuki wa Shauli na mkuki ukapiga ukuta. Daudi akakimbia na kutoroka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli akajaribu kumchomea Daudi ukutani kwa huo mkuki wake, lakini Daudi akauepa huo mkuki wa Sauli ukakita ukutani. Usiku ule ule Daudi akakimbia na kuokoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli akajaribu kumchomea Daudi ukutani kwa huo mkuki wake, lakini Daudi akauhepa huo mkuki wa Sauli ukakita ukutani. Usiku ule ule Daudi akakimbia na kuokoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sauli akajaribu kumpiga Daudi hadi ukutani kwa mkuki wake, ila yeye akaponyoka kutoka mbele ya Sauli, nao huo mkuki akaupiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shauli alijaribu kumchoma Daudi kwa mkuki huo, Lakini Daudi alikwepa mkuki wa Shauli na mkuki ukapiga ukuta. Daudi akakimbia na kutoroka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauli akataka kumchoma Dawidi ukutani kwa mkuki, lakini Dawidi akajiepusha, Sauli asimpate, mkuki ukauchoma ukuta tu. Ndipo, Dawidi alipokimbia kwa hivyo, alivyopona. Usiku huo
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sauli akajaribu kumpiga Daudi hata ukutani kwa mkuki wake, ila yeye akaponyoka kutoka mbele ya Sauli, nao huo mkuki akaupiga ukutani; naye Daudi akakimbia, akaokoka usiku ule.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saulo alijaribu kumuchoma Daudi kwa mukuki ule. Lakini Daudi aliepa mukuki wa Saulo na mukuki ukapiga ukuta. Daudi akakimbia na kutoroka.