1 Samuel 19:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usiku huo, Shauli alituma watu nyumbani kwa Daudi wamwangalie kama yuko ili apate kumwua asubuhi. Lakini Mikali, mke wa Daudi akamwambia Daudi, “Kama huyasalimishi maisha yako usiku huu kesho utauawa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli akatuma watu nyumbani mwa Daudi wailinde hiyo nyumba na kumuua asubuhi. Lakini Mikali, mkewe Daudi, akamwonya akisema, “Usipokimbia kuokoa maisha yako usiku huu, kesho utauawa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Sauli akatuma wajumbe mpaka nyumbani kwa Daudi, ili wamvizie na kumwua asubuhi; naye Mikali, mkewe Daudi, akamwambia, akasema, Wewe usipojiponya nafsi yako usiku huu, kesho utauawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usiku huo, Shauli alituma watu nyumbani kwa Daudi wamwangalie kama yuko ili apate kumwua asubuhi. Lakini Mikali, mke wa Daudi akamwambia Daudi, “Kama huyasalimishi maisha yako usiku huu kesho utauawa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli akatuma watu nyumbani mwa Daudi wailinde hiyo nyumba na kumwua asubuhi. Lakini Mikali, mkewe Daudi, akamwonya akisema, “Kama hukukimbia kuokoa maisha yako usiku huu, kesho yake utauawa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli akatuma watu nyumbani mwa Daudi wailinde hiyo nyumba na kumuua asubuhi. Lakini Mikali, mkewe Daudi, akamwonya akisema, “Kama hukukimbia kuokoa maisha yako usiku huu, kesho yake utauawa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Sauli akatuma wajumbe mpaka nyumbani kwa Daudi, ili wamvizie na kumwua asubuhi; naye Mikali, mkewe Daudi, akamwambia, akasema, Wewe usipojiponya nafsi yako usiku huu, kesho utauawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usiku huo, Shauli alituma watu nyumbani kwa Daudi wamwangalie kama yuko ili apate kumwua asubuhi. Lakini Mikali, mke wa Daudi akamwambia Daudi, “Kama huyasalimishi maisha yako usiku huu kesho utauawa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauli akatuma wajumbe kwenda kuivizia nyumba ya Dawidi, wapate kumwua asubuhi. Lakini mkewe Mikali akampasha Dawidi habari kwamba: Usipojiponya usiku huu, utauawa kesho!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Sauli akatuma wajumbe mpaka nyumbani kwa Daudi, ili wamvizie na kumwua asubuhi; naye Mikali, mkewe Daudi, akamwambia, akasema, Wewe usipojiponya nafsi yako usiku huu, kesho utauawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usiku ule, Saulo akatuma watu kwenye nyumba ya Daudi wamwangalie kama yuko kusudi apate kumwua asubui. Lakini Mikali muke wa Daudi akamwambia Daudi: “Kama hauopoi maisha yako usiku huu, kesho utauawa.”