1 Samuel 19:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Shauli alipopeleka watu wakamkamate. Lakini walipolikuta kundi la manabii likitabiri na Samueli akiliongoza, roho ya Mungu iliwajia wale watumishi wa Shauli, nao pia wakaanza kutabiri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Sauli akatuma watu kumkamata Daudi, lakini walipoona kundi la manabii wakitoa unabii, wakiwa pamoja na Samweli akiwa amesimama hapo kama kiongozi wao, Roho wa Mungu akaja juu ya watu wa Sauli, nao pia wakatoa unabii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamaa ya manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, roho ya Mungu ikawajilia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Shauli alipopeleka watu wakamkamate. Lakini walipolikuta kundi la manabii likitabiri na Samueli akiliongoza, roho ya Mungu iliwajia wale watumishi wa Shauli, nao pia wakaanza kutabiri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Sauli akatuma watu kumkamata, lakini walipoona kundi la manabii wakitoa unabii, wakiwa pamoja na Samweli akiwa amesimama hapo kama kiongozi wao, Roho wa Mungu akaja juu ya watu wa Sauli nao pia wakatoa unabii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Sauli akatuma watu kumkamata Daudi, lakini walipoona kundi la manabii wakitoa unabii, wakiwa pamoja na Samweli akiwa amesimama hapo kama kiongozi wao, Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya watu wa Sauli, nao pia wakatoa unabii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamaa ya manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, Roho ya Mungu ikawajia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Shauli alipopeleka watu wakamkamate. Lakini walipolikuta kundi la manabii likitabiri na Samueli akiliongoza, roho ya Mungu iliwajia wale watumishi wa Shauli, nao pia wakaanza kutabiri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Sauli alipotuma wajumbe kumchukua Dawidi. Hao walipoona kundi la wafumbuaji wakifumbua mambo, naye Samweli akisimama kwao kama kiongozi wao, ndipo, roho ya Mungu ilipowajia wajumbe wa Sauli, nao wakafumbua mambo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Sauli akatuma wajumbe ili kumkamata Daudi; nao hapo walipowaona jamaa ya manabii wakitabiri, na Samweli amesimama kama mkuu wao, roho ya Mungu ikawajilia wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo Saulo akatuma watu kwenda kumukamata. Lakini walipokuta kundi la manabii likitabiri na Samweli akiliongoza, Roho wa Mungu aliwafikia wale watumishi wa Saulo, nao vilevile wakaanza kutabiri.