1 Samuel 19:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipomuua yule Mfilisti Goliathi, alihatarisha maisha yake, naye Mwenyezi-Mungu aliwapa Waisraeli ushindi mkubwa. Wewe ulipoona jambo lile ulifurahi. Kwa nini unataka kutenda dhambi kwa kumwaga damu isiyo na hatia kwa kumwua Daudi bila sababu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alihatarisha maisha yake alipomuua yule Mfilisti. Mwenyezi Mungu akajipatia ushindi mkubwa kwa ajili ya Israeli wote, nawe uliuona na ukafurahi. Kwa nini basi utende mabaya kwa mtu asiye na hatia kama Daudi kwa kumuua bila sababu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa alitia uhai wake mkononi mwake, na kumpiga yule Mfilisti, naye Bwana akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipomuua yule Mfilisti Goliathi, alihatarisha maisha yake, naye Mwenyezi-Mungu aliwapa Waisraeli ushindi mkubwa. Wewe ulipoona jambo lile ulifurahi. Kwa nini unataka kutenda dhambi kwa kumwaga damu isiyo na hatia kwa kumwua Daudi bila sababu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alihatarisha maisha yake alipomwua yule Mfilisti. BWANA akajipatia ushindi mkubwa kwa ajili ya Israeli wote, nawe uliuona na ukafurahi. Kwa nini basi utende mabaya kwa mtu asiye na hatia kama Daudi kwa kumwua bila sababu?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alihatarisha maisha yake alipomuua yule Mfilisti. bwana akajipatia ushindi mkubwa kwa ajili ya Israeli wote, nawe uliuona na ukafurahi. Kwa nini basi utende mabaya kwa mtu asiye na hatia kama Daudi kwa kumuua bila sababu?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa alihatarisha maisha yake, na kumpiga yule Mfilisti, naye BWANA akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipomuua yule Mfilisti Goliathi, alihatarisha maisha yake, naye Mwenyezi-Mungu aliwapa Waisraeli ushindi mkubwa. Wewe ulipoona jambo lile ulifurahi. Kwa nini unataka kutenda dhambi kwa kumwaga damu isiyo na hatia kwa kumwua Daudi bila sababu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwenda kumwua yule Mfilisti alijitoa mwenyewe; ndipo, Bwana alipowapatia Waisiraeli wote wokovu mkubwa, nawe ukaviona, ukafurahi. Mbona unataka kujikosesha kwa kumwaga damu ya mtu asiyekosa ukimwua Dawidi bure tu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa alitia uhai wake mkononi mwake, na kumpiga yule Mfilisti, naye BWANA akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipomwua yule Mufilistini Goliati, alihatarisha maisha yake, naye Yawe aliwapa Waisraeli ushindi mukubwa. Wewe ulipoona jambo lile ulifurahi. Kwa nini unataka kutenda zambi kwa kumwanga damu isiyokuwa na kosa kwa kumwua Daudi bila sababu?”