1 Samuel 2:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maadui wa Mwenyezi-Mungu watavunjwa vipandevipande; atanguruma dhidi yao kama radi mbinguni. Mwenyezi-Mungu ataihukumu dunia yote; atampa nguvu mfalme wake ataukuza uwezo wa mteule wake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wale wampingao Mwenyezi Mungu wataharibiwa kabisa. Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni; Mwenyezi Mungu ataihukumu miisho ya dunia. “Atampa nguvu mfalme wake, na kuitukuza pembe ya mpakwa mafuta wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maadui wa Mwenyezi-Mungu watavunjwa vipandevipande; atanguruma dhidi yao kama radi mbinguni. Mwenyezi-Mungu ataihukumu dunia yote; atampa nguvu mfalme wake ataukuza uwezo wa mteule wake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wale wampingao BWANA wataharibiwa kabisa. Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni; BWANA ataihukumu miisho ya dunia. “Atampa nguvu mfalme wake, na kuitukuza pembe ya mpakwa mafuta wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wale wampingao bwana wataharibiwa kabisa. Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni; bwana ataihukumu miisho ya dunia. “Atampa nguvu mfalme wake, na kuitukuza pembe ya mpakwa mafuta wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maadui wa Mwenyezi-Mungu watavunjwa vipandevipande; atanguruma dhidi yao kama radi mbinguni. Mwenyezi-Mungu ataihukumu dunia yote; atampa nguvu mfalme wake ataukuza uwezo wa mteule wake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakaoshindana na Bwana watapondwa, atakapovumisha ngurumo juu yao mbinguni. Bwana atayahukumu mapeo ya nchi, naye mfalme wake atampa uwezo atakapoitukuza pembe yake yeye, aliyempaka mafuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waadui za Yawe watavunjwa vipandevipande; atanguruma juu yao kama radi mbinguni. Yawe ataihukumu dunia yote, atamupa nguvu mufalme wake, na atautukuza uwezo wa muchaguliwa wake.