1 Samuel 2:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Eli aliwabariki Elkana na mkewe, akisema, “Mwenyezi-Mungu na akupe wewe Elkana watoto wengine kwa mwanamke huyu ili wachukue mahali pa yule uliyempa Mwenyezi-Mungu.” Kisha wao hurudi nyumbani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Eli alikuwa akiwabariki Elkana na mkewe, akisema, “Mwenyezi Mungu na akupe watoto kwa mwanamke huyu ili kuchukua nafasi ya yule aliyekuwa amemwomba na akamtoa kwa Mwenyezi Mungu.” Kisha wakawa wanaenda nyumbani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Eli akambariki Elkana na mkewe, akasema, Bwana na akupe uzao kwa mwanamke huyu, badala ya azimo aliloazimiwa Bwana. Kisha wakaenda nyumbani kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Eli aliwabariki Elkana na mkewe, akisema, “Mwenyezi-Mungu na akupe wewe Elkana watoto wengine kwa mwanamke huyu ili wachukue mahali pa yule uliyempa Mwenyezi-Mungu.” Kisha wao hurudi nyumbani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Eli alikuwa akiwabariki Elikana na mkewe, akisema, “BWANA na akupe watoto kwa mwanamke huyu ili kuchukua nafasi ya yule aliyekuwa amemwomba na akamtoa kwa BWANA.” Kisha wakawa wanakwenda nyumbani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Eli alikuwa akiwabariki Elikana na mkewe, akisema, “ bwana na akupe watoto kwa mwanamke huyu ili kuchukua nafasi ya yule aliyekuwa amemwomba na akamtoa kwa bwana.” Kisha wakawa wanakwenda nyumbani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Eli akambariki Elkana na mkewe, akasema, BWANA na akupe uzao kwa mwanamke huyu, wachukue mahali pa yule aliyemtoa kwa BWANA. Kisha wakarudi nyumbani kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Eli aliwabariki Elkana na mkewe, akisema, “Mwenyezi-Mungu na akupe wewe Elkana watoto wengine kwa mwanamke huyu ili wachukue mahali pa yule uliyempa Mwenyezi-Mungu.” Kisha wao hurudi nyumbani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Eli akambariki Elkana na mkewe akisema: Bwana na akupatie kizazi kwake mwanamke huyu cha kumlipa ombo lake, alilomwomba Bwana! Kisha wakaenda zao kufika kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Eli akambariki Elkana na mkewe, akasema, BWANA na akupe uzao kwa mwanamke huyu, badala ya azimo aliloazimiwa BWANA. Kisha wakaenda nyumbani kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Eli aliwabariki Elekana na muke wake, akisema: “Yawe akupe wewe Elekana watoto wengine kwa mwanamuke huyu kusudi wakamate nafasi ya yule uliyemupa Yawe.” Kisha wao walirudi kwao.