1 Samuel 2:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu akimkosea mwenzake, anaweza kuombewa kwa Mungu, ili Mungu amsamehe. Lakini mtu akimkosea Mwenyezi-Mungu nani awezaye kumwombea msamaha?” Lakini watoto hao hawakumsikiliza baba yao, kwani Mwenyezi-Mungu alikwisha kata shauri kuwaua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu akifanya dhambi dhidi ya mtu mwenzake, mtu mwingine aweza kumwombea kwa Mungu, lakini kama mtu akimfanyia Mungu dhambi, ni nani atakayemwombea?” Hata hivyo wanawe hawakusikia maonyo ya baba yao, kwa sababu Mwenyezi Mungu alitaka kuwaua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa Bwana, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu Bwana amekusudia kuwaua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu akimkosea mwenzake, anaweza kuombewa kwa Mungu, ili Mungu amsamehe. Lakini mtu akimkosea Mwenyezi-Mungu nani awezaye kumwombea msamaha?” Lakini watoto hao hawakumsikiliza baba yao, kwani Mwenyezi-Mungu alikwisha kata shauri kuwaua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mtu akifanya dhambi dhidi ya mtu mwenzake, mtu mwingine aweza kumwombea kwa Mungu, lakini kama mtu akimfanyia Mungu dhambi, ni nani atakayemwombea?” Hata hivyo wanawe hawakusikia maonyo ya baba yao, kwa sababu BWANA alitaka kuwaua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mtu akifanya dhambi dhidi ya mtu mwenzake, mtu mwingine aweza kumwombea kwa Mungu, lakini kama mtu akimfanyia Mungu dhambi, ni nani atakayemwombea?” Hata hivyo wanawe hawakusikia maonyo ya baba yao, kwa sababu bwana alitaka kuwaua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu mmoja akimkosea mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosea BWANA, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu BWANA amekusudia kuwaua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu akimkosea mwenzake, anaweza kuombewa kwa Mungu, ili Mungu amsamehe. Lakini mtu akimkosea Mwenyezi-Mungu nani awezaye kumwombea msamaha?” Lakini watoto hao hawakumsikiliza baba yao, kwani Mwenyezi-Mungu alikwisha kata shauri kuwaua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akimkosea mtu mwenziwe, Mungu atampatiliza, lakini akimkosea Bwana, yuko nani atakayemwombea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwani Bwana alitaka kuwaua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa BWANA, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu BWANA amekusudia kuwaua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu akimukosea mwenzake, anaweza kuombewa kwa Mungu, kusudi Mungu amusamehe. Lakini mutu akimukosea Yawe nani anayeweza kumwombea musamaha?” Lakini watoto hao hawakumusikiliza baba yao, maana Yawe alikwisha kata shauri la kuwaua.