1 Samuel 2:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kati ya makabila yote ya Israeli nilimchagua Aroni na jamaa yake kuwa makuhani wangu, wanitumikie madhabahuni, wafukize ubani na kuvaa kizibao mbele yangu. Nikaipatia jamaa ya mzee wako tambiko zangu ambazo Waisraeli walinitolea kwa moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilimchagua baba yako kati ya makabila yote ya Israeli kuwa kuhani wangu, kukwea kwenye madhabahu yangu, kufukiza uvumba na kuvaa kizibau mbele yangu. Pia niliwapa nyumba ya baba yako sadaka zote zilizotolewa kwa moto na Waisraeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Sikumchagua yeye katika kabila zote za Israeli, ili awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu; na kufukiza uvumba, na kuvaa naivera mbele zangu? Nami sikuwapa watu wa mbari ya baba yako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kati ya makabila yote ya Israeli nilimchagua Aroni na jamaa yake kuwa makuhani wangu, wanitumikie madhabahuni, wafukize ubani na kuvaa kizibao mbele yangu. Nikaipatia jamaa ya mzee wako tambiko zangu ambazo Waisraeli walinitolea kwa moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilimchagua baba yako kati ya makabila yote ya Israeli kuwa kuhani wangu, kukwea kwenye madhabahu yangu, kufukiza uvumba na kuvaa kisibau mbele yangu. Pia niliwapa nyumba ya baba yako sadaka zote zilizotolewa kwa moto na Waisraeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilimchagua baba yako kati ya makabila yote ya Israeli kuwa kuhani wangu, kukwea kwenye madhabahu yangu, kufukiza uvumba na kuvaa kisibau mbele yangu. Pia niliwapa nyumba ya baba yako sadaka zote zilizotolewa kwa moto na Waisraeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Sikumchagua yeye katika makabila yote za Israeli, ili awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu; na kufukiza uvumba, na kuvaa naivera mbele zangu? Nami sikuwapa watu wa koo za baba yako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kati ya makabila yote ya Israeli nilimchagua Aroni na jamaa yake kuwa makuhani wangu, wanitumikie madhabahuni, wafukize ubani na kuvaa kizibao mbele yangu. Nikaipatia jamaa ya mzee wako tambiko zangu ambazo Waisraeli walinitolea kwa moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikauchagua katika mashina yote ya Waisiraeli kuwa watambikaji, wapande pangu pa kutambikia na kuvukiza uvumba na kuvaa kisibau cha mtambikaji mbele yangu, nikaupa mlango wa baba yako ng'ombe zote za tambiko, wana wa Isiraeli wanazozitoa za kuteketezwa motoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Sikumchagua yeye katika kabila zote za Israeli, ili awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu; na kufukiza uvumba, na kuvaa naivera mbele zangu? Nami sikuwapa watu wa mbari ya baba yako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati ya makabila yote ya Israeli nilimuchagua Haruni na jamaa yake kuwa makuhani wangu, wanitumikie kwenye mazabahu, wafukize ubani na kuvaa kizibao mbele yangu. Nikaipatia jamaa ya babu yako sadaka zangu ambazo Waisraeli walinitolea kwa moto.