1 Samuel 2:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, nitajiinulia kuhani mwingine mwaminifu atakayefanya kulingana na yale yaliyomo moyoni na akilini mwangu. Nitamjengea ukoo imara, naye atahudumu daima mbele ya mfalme wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi mwenyewe nitajiinulia kuhani mwaminifu, ambaye atafanya sawasawa na kile kilichoko moyoni mwangu na akilini mwangu. Nitaiimarisha nyumba yake ya ukuhani, naye atahudumu mbele ya mpakwa mafuta wangu daima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika nia yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, nitajiinulia kuhani mwingine mwaminifu atakayefanya kulingana na yale yaliyomo moyoni na akilini mwangu. Nitamjengea ukoo imara, naye atahudumu daima mbele ya mfalme wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi mwenyewe nitajiinulia kuhani mwaminifu, ambaye atafanya sawasawa na kile kilichoko moyoni mwangu na akilini mwangu. Nitaifanya nyumba yake kuwa imara, naye atahudumu mbele ya mpakwa mafuta wangu daima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi mwenyewe nitajiinulia kuhani mwaminifu, ambaye atafanya sawasawa na kile kilichoko moyoni mwangu na akilini mwangu. Nitaifanya nyumba yake kuwa imara, naye atahudumu mbele ya mpakwa mafuta wangu daima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya kulingana na yale yaliyo katika moyo wangu na katika akili yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, nitajiinulia kuhani mwingine mwaminifu atakayefanya kulingana na yale yaliyomo moyoni na akilini mwangu. Nitamjengea ukoo imara, naye atahudumu daima mbele ya mfalme wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha nitajiinulia mtambikaji mwelekevu atakayeyafanya mapenzi ya moyo wangu na ya Roho yangu; yeye nitamjengea nyumba ya kweli, aendelee siku zote machoni pake yule, nitakayempaka mafuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika nia yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, nitajiinulia kuhani mwingine mwaminifu atakayefanya kulingana na yale yanayokuwa ndani ya moyo na akili yangu. Nitamujengea ukoo imara, naye atatumika siku zote mbele ya mufalme wangu muchaguliwa.