1 Samuel 2:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale ambao zamani walikuwa na chakula tele, sasa wanaajiriwa ili wapate chakula. Lakini waliokuwa na njaa, sasa hawana njaa tena. Mwanamke tasa amejifungua watoto saba. Lakini mama mwenye watoto wengi, sasa ameachwa bila mtoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe ili kupata chakula, lakini wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Mwanamke yule aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini yule aliyekuwa na wana wengi amedhoofika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale ambao zamani walikuwa na chakula tele, sasa wanaajiriwa ili wapate chakula. Lakini waliokuwa na njaa, sasa hawana njaa tena. Mwanamke tasa amejifungua watoto saba. Lakini mama mwenye watoto wengi, sasa ameachwa bila mtoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe ili kupata chakula, lakini wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Mwanamke yule aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi amedhoofika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe ili kupata chakula, lakini wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Mwanamke yule aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi amedhoofika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Lakini waliokuwa na njaa sasa hawana njaa tena. Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini aliye na watoto wengi amehuzunika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale ambao zamani walikuwa na chakula tele, sasa wanaajiriwa ili wapate chakula. Lakini waliokuwa na njaa, sasa hawana njaa tena. Mwanamke tasa amejifungua watoto saba. Lakini mama mwenye watoto wengi, sasa ameachwa bila mtoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walioshiba hufanya kazi, wapate chakula tu, lakini waliokuwa wenye njaa, njaa zao hukoma kabisa, mwanamke mgumba huzaa watoto saba, naye mwenye wana wengi hufifia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale ambao zamani walikuwa na chakula tele, sasa wanafanya kazi wapate chakula. Lakini waliokuwa na njaa, sasa hawana njaa tena. Mwanamuke tasa, amezaa watoto saba. Lakini mama mwenye watoto wengi, sasa ameachwa bila mutoto.