1 Samuel 20:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yonathani akamwambia Daudi, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, na awe shahidi yetu. Kesho au kesho kutwa, wakati kama huu nitamwuliza baba yangu. Ikiwa msimamo wake juu yako ni mzuri nitakueleza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Ninakuahidi kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, hakika nitamchunguza baba yangu wakati kama huu kesho kutwa! Kama ameweka utaratibu wa kufaa kukuhusu wewe, je, sitakutumia ujumbe na kukufahamisha?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yonathani akamwambia Daudi, Bwana, Mungu wa Israeli, na awe shahidi; nitakapokuwa nimekwisha kumwuliza baba yangu, kama wakati huu kesho, au siku ya tatu, angalia, kama liko neno jema la kumfaa Daudi, je! Nisikupelekee habari na kukufunulia neno hili?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yonathani akamwambia Daudi, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, na awe shahidi yetu. Kesho au kesho kutwa, wakati kama huu nitamwuliza baba yangu. Ikiwa msimamo wake juu yako ni mzuri nitakueleza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Ninakuahidi kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli hakika nitamchunguza baba yangu wakati kama huu kesho kutwa! Kama ameweka utaratibu wa kufaa kukuhusu wewe, je, sitakutumia ujumbe na kukufahamisha?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Ninakuahidi kwa jina la bwana, Mungu wa Israeli, hakika nitamchunguza baba yangu wakati kama huu kesho kutwa! Kama ameweka utaratibu wa kufaa kukuhusu wewe, je, sitakutumia ujumbe na kukufahamisha?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yonathani akamwambia Daudi, BWANA, Mungu wa Israeli, na awe shahidi; nitakapokuwa nimekwisha kumwuliza baba yangu, kama wakati huu kesho, au siku ya tatu, angalia, kama liko neno jema la kumfaa Daudi, je! Nisikupelekee habari na kukufunulia neno hili?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yonathani akamwambia Daudi, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, na awe shahidi yetu. Kesho au kesho kutwa, wakati kama huu nitamwuliza baba yangu. Ikiwa msimamo wake juu yako ni mzuri nitakueleza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yonatani akamwambia Dawidi: Bwana Mungu wa Isiraeli ni shahidi! Kesho wakati kama huu au kesho kutwa nikimchunguza baba yangu na kuona, ya kuwa anayo mema ya kumfanyizia Dawidi, basi, nisipotuma mtu kwako, niyafunue masikioni pako,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yonathani akamwambia Daudi, BWANA, Mungu wa Israeli, na awe shahidi; nitakapokuwa nimekwisha kumwuliza baba yangu, kama wakati huu kesho, au siku ya tatu, angalia, kama liko neno jema la kumfaa Daudi, je! Nisikupelekee habari na kukufunulia neno hili?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yonatani akamwambia Daudi: “Yawe, Mungu wa Israeli, akuwe mushuhuda kati yetu. Kesho au kesho kutwa, wakati kama huu nitamwuliza baba yangu. Ikiwa musimamo wake juu yako ni muzuri nitakuelezea.