1 Samuel 20:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu na aniue ikiwa Shauli anakusudia kukudhuru, nami nisikutahadharishe ili uende mahali mbali ambapo utakuwa salama. Mwenyezi-Mungu na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, Mwenyezi Mungu na aniadhibu vikali zaidi iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende salama. Mwenyezi Mungu na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukupeleka uende zako kwa amani; na Bwana awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu na aniue ikiwa Shauli anakusudia kukudhuru, nami nisikutahadharishe ili uende mahali mbali ambapo utakuwa salama. Mwenyezi-Mungu na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, BWANA na anishughulikie tena iwe kwa ukali, iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende kwa salama. BWANA na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, bwana na anishughulikie kwa ukali, iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende salama. bwana na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukutuma uende zako kwa amani; na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu na aniue ikiwa Shauli anakusudia kukudhuru, nami nisikutahadharishe ili uende mahali mbali ambapo utakuwa salama. Mwenyezi-Mungu na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana na aendelee kumfanyizia Yonatani hivi na hivi! Lakini baba yangu akiona kuwa vema kukufanyizia mabaya, nitayafunua nayo masikioni pako, upate kwenda zako na kutengemana; naye Bwana awe na wewe, kama alivyokuwa na baba yangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukupeleka uende zako kwa amani; na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe aniue ikiwa Saulo anakusudia kukuzuru nami nisipokujulisha kusudi uende pahali pa mbali ambapo utakuwa salama. Yawe akuwe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.