1 Samuel 20:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama ilivyokuwa kawaida yake, mfalme aliketi kwenye kiti chake kilichokuwa karibu ukutani. Yonathani akaketi mkabala na mfalme na Abneri akaketi karibu na mfalme. Lakini mahali pa Daudi pakawa wazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaketi mahali pake pa kawaida karibu na ukuta, kuelekeana na Yonathani, naye Abneri akaketi karibu na Mfalme Sauli, lakini kiti cha Daudi kilikuwa wazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme aliketi kitini mwake kama sikuzote, katika kiti kilichokuwa karibu na ukuta; Yonathani alikuwa mbele yake; Abneri naye akaketi karibu na Sauli; lakini mahali pake Daudi palikuwa hapana mtu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama ilivyokuwa kawaida yake, mfalme aliketi kwenye kiti chake kilichokuwa karibu ukutani. Yonathani akaketi mkabala na mfalme na Abneri akaketi karibu na mfalme. Lakini mahali pa Daudi pakawa wazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaketi mahali pake pa kawaida karibu na ukuta, kuelekeana na Yonathani, naye Abneri akaketi karibu na Mfalme Sauli, lakini kiti cha Daudi kilikuwa wazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaketi mahali pake pa kawaida karibu na ukuta, kuelekeana na Yonathani, naye Abneri akaketi karibu na Mfalme Sauli, lakini kiti cha Daudi kilikuwa wazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme aliketi kitini mwake kama siku zote, katika kiti kilichokuwa karibu na ukuta; Yonathani alikuwa mbele yake; Abneri naye akaketi karibu na Sauli; lakini mahali pake Daudi palikuwa hapana mtu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama ilivyokuwa kawaida yake, mfalme aliketi kwenye kiti chake kilichokuwa karibu ukutani. Yonathani akaketi mkabala na mfalme na Abneri akaketi karibu na mfalme. Lakini mahali pa Daudi pakawa wazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mfalme akakaa mahali pake pa siku zote, ni hapo ukutani; naye Yonatani akaja kusimama hapo, naye Abineri akakaa kando yake Sauli; lakini kiti chake Dawidi kikawa hakina mtu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme aliketi kitini mwake kama sikuzote, katika kiti kilichokuwa karibu na ukuta; Yonathani alikuwa mbele yake; Abneri naye akaketi karibu na Sauli; lakini mahali pake Daudi palikuwa hapana mtu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama ilivyokuwa kawaida yake, mufalme aliikaa kwenye kiti chake kilichokuwa karibu na ukuta. Yonatani akaikaa mbele kuelekea mufalme na Abeneri akaikaa karibu na mufalme. Lakini nafasi ya Daudi ikakuwa wazi.